Wanajeshi wa Japan / Photo: AP

Japan inajiandaa kuwaokoa raia wake kutoka Sudan iliyokumbwa na vita, maafisa walisema Jumatano.

Hirokazu Matsuno, msemaji wa serikali, alisema kwenye mahojiano na waandishi wa habari kwamba wafanyakazi kutoka Jeshi la Kujilinda la Japan (SDF) watatumwa katika taifa hilo la Afrika kuwaokoa raia wa Japan.

Kuna takriban raia 60 wa Japan wanaoishi nchini Sudan ambayo imeshuhudia mapigano ya wanamgambo tangu wikiendi iliyopita.

Matsuno alisema "hakuna ripoti za majeraha" kati ya watu wa Japan wanaoishi Sudan, Kyodo News yenye makao yake Tokyo iliripoti.

Mapigano yalizuka siku ya Jumamosi kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Rapid Support Forces, RSF, vya kijeshi katika mji mkuu Khartoum na pembezoni. Pande hizo mbili zimekubaliana kusitisha mapigano kwa masaa 24.

Zaidi ya watu 180 wameuawa na wengine 1,800 kujeruhiwa katika ghasia zinazoendelea, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

AA