Chanjo ya malaria inayo tazamwa kwa makini kutoka Chuo Kikuu cha Oxford imepata kibali chake cha kwanza, nchini Ghana.
Juhudi hizo ni mojawapo ya juhudi zinazolenga kukabiliana na ugonjwa huo unaoua zaidi ya watu 600,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa watoto barani Afrika. Muundo mgumu na mzunguko wa maisha wa vimelea vya malaria kwa muda mrefu umezuia juhudi za kutengeneza chanjo.
Baada ya miongo kadhaa ya kazi, chanjo ya kwanza ya malaria, Mosquirix kutoka kampuni ya dawa ya Uingereza, GSK, iliidhinishwa mwaka jana na Shirika la Afya Duniani (WHO), lakini ukosefu wa fedha na uwezo wa kibiashara umezuia uwezo wa kampuni hiyo kuzalisha dozi nyingi zaidi zinazohitajika.
Chanjo ya Oxford, ambayo imepata idhini ya udhibiti katika kundi la watoto wenye umri wa miezi 5 hadi miezi 36 - ina faida ya utengenezaji kutokana na mpango na Taasisi ya Serum ya India kuzalisha hadi dozi milioni 200 kila mwaka. .
Kinyume chake, GSK imejitolea kuzalisha hadi dozi milioni 15 za Mosquirix kila mwaka hadi 2028, chini ya takribani dozi milioni 100 kwa mwaka za chanjo ya dozi nne ambazo WHO inasema zinahitajika kwa muda mrefu kuhudumia takriban watoto milioni 25.
Data ya hatua ya kati kutoka katika jaribio la chanjo ya Oxford iliyo husisha zaidi ya watoto wachanga 400 ilichapishwa katika jarida la matibabu mnamo mwezi Septemba.
Ufanisi wa chanjo ulikuwa kwa asilimia 80% katika kikundi kilichopokea kipimo cha juu cha chanjo ya kuongeza kinga, na 70% katika kikundi cha wasaidizi wa dozi ya chini, katika miezi 12 kufuatia dozi ya nne. Dozi hizo zilitolewa kabla ya msimu wa kilele wa malaria nchini Burkina Faso.
Data kutoka kwa majaribio ya kimatibabu ya awamu ya Tatu nchini Burkina Faso, Kenya, Mali na Tanzania ambayo yameandikisha watoto 4,800 inatarajiwa kuchapishwa katika jarida la matibabu katika miezi ijayo.
Chanjo za watoto barani Afrika kwa kawaida hulipiwa na mashirika ya kimataifa kama vile Gavi na UNICEF baada ya kuungwa mkono na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO).
Hii ni mara ya kwanza kwa chanjo kuu kuidhinishwa kwanza katika nchi ya Kiafrika, kabla ya mataifa tajiri, Hill aliongeza, akibainisha kuwa haikuwa kawaida kwamba mamlaka ya udhibiti barani Afrika imepitia data hiyo haraka kuliko WHO.
"Hasa tangu COVID, wasimamizi wa Kiafrika wamekuwa wakichukua msimamo mkali zaidi, wamekuwa wakisema...hatutaki kuwa wa mwisho kwenye foleni."