Waziri wa mambo ya nje wa Ghana Shirley Ayorkor Botchwey amesema Ghana iko kwenye mchakato wa kuchora mipango juu ya jambo hilo kabla ya kuchukua hatua kamili.
Ghana inatarajiwa kujiunga na Rwanda, Gambia, Benin na Shelisheli ambazo ni nchi za Afrika ambazo zimeondoa vikwazo hivyo vya usafiri kwa raia wa mataifa ya Afrika.
Waziri amesema kuwa, kusafiri bila visa kati ya nchi za afrika pia kutakuwa na faida kubwa kwa sekta ya utalii ya Ghana.
Wizara husika za Ghana za utalii, usalama wa ndani na mambo ya nje, yanaendelea na mikakati ya kuona namna ya kufanikisha uondoaji wa mahitaji ya visa kuingia Ghana.
Hivi karibuni, Serikali za Ghana na Afrika Kusini zilitia saini makubaliano ya kuondoa visa ambayo yalianza kutumika tarehe 1 Novemba 2023.
Hii inaruhusu Waafrika Kusini na Waghana kuomba visa zao mtandaoni.
Chini ya makubaliano hayo, raia wa Ghana, wataruhusiwa kukaa Afrika Kusini kwa muda wa siku 90 bila visa.
Iwapo Ghana itaendelea na utekelezaji wa kuondoa mahitaji ya visa, itaimarisha zaidi msimamo wa nchi hiyo kama mtetezi anayeshabikia utangamano barani.