Tiwa Savage

Mwimbaji wa Nigeria Tiwa Savage anasema filamu yake mpya, 'Water and Garri,' inavuma kwenye chati za juu katika nchi 14 barani Afrika na kwengineko.

Tiwa, ambaye jina lake kamili ni Tiwatope Omolara Savage, alichapisha ujumbe wa kusherehekea mafanikio ya filamu yake kwenye mtandao wa X, ambayo inasikika kwenye Prime Video.

"Kumi bora kati ya nchi 14. Shukrani kwa familia ya WAG (Water And Garri) duniani kote kwa upendo na usaidizi," Savage alisema katika ujumbe wake.

'Water and Garri,' iliyotayarishwa na Savage na mtengenezaji wa filamu kutoka Nigeria Jimi Adesanya, ilizinduliwa kwenye Prime Video Ijumaa, Mei 10, 2024.

Kulingana na Tiwa, 'Water and Garri' inavuma nchini Nigeria, Ghana, Cameroon, Jamhuri ya Benin, Rwanda, Togo, Georgia, Zambia, Cyprus, Uganda, Ukraine, Tanzania, Qatar, na Afrika Kusini.

Filamu hiyo inafuatia hadithi ya Aisha (iliyoigizwa na Savage), mbunifu mahiri wa mitindo ambaye anarudi katika mji aliozaliwa baada ya kuishi miaka mingi huko Marekani. Lakini baada ya kuwasili Aisha anagundua kwamba nyumbani kumebadilika na sasa kumejaa vurugu na mvutano.

Filamu hiyo, iliyoongozwa na Meji Alabi, ilirikodiwa huko Cape Coast, Ghana, na imewashirikisha Mike Afolarin, Andrew Bunting, na Jemima Osunde.

TRT Afrika