FIFA imezindua rasmi kombe jipya la FIFA Club World Cup Novemba 14, 2024. /Picha: Fifa

FIFA imezindua rasmi kombe jipya la FIFA Club World Cup Novemba 14, 2024, ambalo FIFA imesema, lina muundo wa kisasa unaowakilisha umahiri na mshikamano wa vilabu bora ulimwenguni.

Imeongeza kusema kuwa, ubunifu wake una vipengele vya thamani vinavyolenga kuimarisha hadhi ya mashindano hayo.

Limetengezwa kwa dhahabu karati 24, na maandiko, michoro na alama zinazowakilisha matukio muhimu katika historia ya soka. Aidha kombe hilo limetengenzwa kwa ushirikiano na Tiffany & Co.

Pamoja na uzinduzi huo, mfumo wa FIFA Club World Cup pia umeboreshwa ili kuhusisha timu 32, ikilinganishwa na timu 7 za awali.

Mashindano haya mapya yatafanyika kila baada ya miaka minne, sawa na Kombe la Dunia kwa timu za taifa, na yataanza rasmi mwaka 2025 huko Marekani.

Mfumo huu unalenga kuleta ushindani zaidi na kuongeza hamasa kwa mashabiki wa vilabu vya mpira kote duniani.

TRT Afrika