Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo ya simu na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis.
Rais Erdogan alimpongeza Waziri Mkuu wa Ugiriki Mitsotakis katika siku yake ya kuzaliwa, kurugenzi ya mawasiliano ya Uturuki ilisema siku ya Jumatatu.
Uhusiano wa Uturuki na Ugiriki, ulitawaliwa na uhasama wa muda mrefu, lakini hali ilibadilika mwaka jana kufuatia matetemeko pacha yaliyoikumba kusini mwa Uturuki.
Madhara ya maafa hayo yaliilazimu Uturuki kutuma salamu za rambirambi pamoja na kutoa msaada wa kibinadamu, kama aina ya mshikamano. Ishara hiyo, kutoka serikali na umma wa Ugiriki ulipokelewa vyema na Uturuki, na kuanzisha mazungumzo kati ya washirika hao wa NATO.
Ungezeko la Kidiplomasia
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis walitumia fursa hiyo kuimarisha uhusiano wakati wa mkutano wao Julai 12 katika Mkutano wa NATO huko Vilnius.
Huu ulikuwa ni mkutano wao wa kwanza ndani ya miezi 16. Ulionesha nia ya dhati ya mwanzo mpya, na kutangaza kurejesha baraza la juu la ushirikiano kati ya Ugiriki na Uturuki, na kupanga mkutano wake wa tano katika kipindi cha 2023, baada ya kutokufanyika kwa miaka saba.
Kuimarisha zaidi kasi hiyo nzuri, Erdogan na Mitsotakis walikutana tena mjini New York Septemba 20, siku 15 tu baada ya mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan na mwenzake wa Ugiriki George Gerapetritis mjini Ankara.
Wakati wa mkutano huu, viongozi walijishughulisha na hali ya sasa ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili, walijadili matarajio, na kushughulikia maswala ya pande zote kama vile changomoto ya mabadiliko ya tabia nchi, uhamiaji usio wa kawaida, na maswala ya kikanda na kimataifa.
Ziara ya Erdogan mjini Athens
Mwezi Desemba, Rais wa Uturuki Erdogan alikutana na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis katika ziara yake ya siku moja nchini Ugiriki.
Katika mkutano huu, nchi zote mbili zilitangaza "Tamko la Athens kuhusu Mahusiano ya Kirafiki na Ujirani Mwema."
Uturuki, ambayo ni mwanachama wa NATO kwa zaidi ya miaka 70, imepinga vitendo vya uchochezi na matamshi ya mara kwa mara ya Ugiriki katika eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja kuvipa silaha baadhi ya visiwa vilivyo karibu na mwambao wa Uturuki visivyo na majeshi chini ya mikataba ya muda mrefu, akisema kwamba hatua hizo zinavuruga juhudi zake za nia njema kuleta amani.
Wakati mazungumzo baina ya nchi hzio mbili yakiendelea, ndivyo zinavyotoka sauti za matumaini na nia thabiti ya kutatua masuala hayo.