DRC: Matatizo ya umeme kuathiri uchumi

DRC: Matatizo ya umeme kuathiri uchumi

DRC inapata mabilioni ya dola kupitia machimbo ya madini
Gems and Minerals / Photo: AP

Katika mkutano na waandishi wa habari, Nicolas Kazadi, Waziri wa Fedha wa Kongo alitangaza ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme kwa gharama ya dola milioni tatu ili kuondokana na matatizo ya umeme ambayo yanaathiri uzalishaji wa almasi katika jimbo la Kasai.

Kauli hii inakuja wakati kampuni ya uchimbaji madini ya Bakwanga, MIBA, ikikumbwa na matatizo kadhaa ya uendeshaji kutokana na matatizo ya umeme na kuharibika kwa vifaa vya zamani ya tangu miaka ya 1960.

DRC inapata mabilioni ya dola kupitia machimbo ya madini

MIBA, ikiwa ni kampuni yenye leseni ya uchimbaji madini ya umma, inachangia zaidi katika uchumi wa taifa na uzalishaji wake wa kila mwaka wa karati milioni 6.

Ina viwanda vitatu vikubwa vya kusindika almasi.

Nafasi yake ina ukubwa wa kilomita za mraba 45 kusini mwa mji wa Mbuji-Mayi na ina akiba ya karati za almasi milioni 66 kutoka kwa hifadhi za kimkakati za nchi.

Kufuatia matatizo ya umeme, MIBA imeona uwezo wake wa uzalishaji kupungua tangu miaka ya 2000.

"MIBA ina madeni makubwa. Inadaiwa na wafanyakazi wake na watoa huduma wa dola milioni mia kadhaa. Hakuna uwekezaji wa madini unaofanywa, ikiwa mtu hana tathmini kamili ya hifadhi ambazo ziko kwenye eneo la chini ya mgodi unaozingatiwa” Waziri Kaizid asema.

Serikali imetangaza kwamba kampuni hii inahitaji dola milioni 453 kuendelea kufanya kazi ndani ya miaka mitano inayofuata.

Kulingana na mamlaka ya MIBA, zana ya uzalishaji imechakaa na ni kama haipo, Mashine za uchimbaji, zilizonunuliwa miaka miwili iliyopita zimeharibika.

Zaidi ya hayo ni ukosefu wa nishati ya umeme katika kiwango cha poligoni ya madini, kufuatia uharibifu uliorekodiwa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika kiwango cha kituo cha kuzalisha umeme cha Tshiala, ambacho lazima hasa kitoe karibu megawati 2.5 kwa poligoni kwa ajili ya uzalishaji wa madini.

Waziri Kazadi anaendelea kuwa kampuni hii ya serikali ina akiba kubwa lakini ambayo haijulikani vya kutosha. "Tumetoa kipaumbele kwa uidhinishaji wa hifadhi katika sehemu hii ya nchi ambayo sio tu ya almasi bali pia nikeli na chromium”.

TRT Afrika