Kikosi cha Kanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mashariki mwa DRC picha na EACCRF / Photo: TRT World

Hatuzungumzii juu ya mzozo nchini Yemen, au mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, wala mzozo wa Israeli na Palestina.

Hapa tunazungumzia janga linaloendelea moyoni mwa Afrika, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mauaji ya raia, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto, ubakaji... kwa ufupi, jinai ya kutisha... Yote haya yanatokea mbali na jicho la kamera na macho ya umma.

Kwa kifupi, vita nchini Congo vilianza mwishoni mwa miaka ya 1990 na bado vinaendelea mpaka sasa, mbele ya jumuiya ya kimataifa, ambayo mpaka sasa imeonyesha udhaifu wake mkubwa katika kutatua migogoro.

Wengi wanajiuliza kwa nini vita nchini Congo havipewi nafasi kuu katika ajenda ya kimataifa, wala hazipewi kipaombele katika vyombo vya habari vya Magharibi?

Fahamu kuwa kuna masuala mengi ya kimkakati yanayohusu vita hivi vinavyoendelea Mashariki mwa Congo. Hasa ni mapambano kati ya makundi yenye silaha yanayofadhiliwa kwa lengo la kudhibiti rasilimali kubwa zilizojaa katika ardhi ya eneo hilo.

Eneo hilo la Congo lina madini yanayohitajika sana na makampuni makubwa ya teknolojia, kama vile coltan ambayo hutumika kutengeneza vichujio vya umeme vya kompyuta, simu za mkononi, na vifaa vyengine vya kisasa.

Lithium, ambayo ni muhimu katika kutengeneza betri za magari ya umeme, bila uzalishaji wa CO2 na inachukuliwa kama mustakabali wa utengezaji wa magari. Pia kuna mbao inayohitajika sana na nchi za Asia, na dhahabu, almasi... Orodha ni ndefu.

Kwa makundi ya waasi kutoka nchi nyingine, kwa kiasi kikubwa, wanazingira eneo hilo kwa miongo kadhaa, madini haya ni muhimu sana. Wamechukua udhibiti wa maeneo makubwa, wakidhibiti vituo vingi vya madini. Kulingana na baadhi ya wachambuzi, wanafadhiliwa na makampuni makubwa yanayoshiriki katika sehemu hii ya Congo.

Wanatumia mzozo huu kunyang'anya rasilimali za chini ya ardhi ya Kongo, na kisha kusafirisha madini hayo kupitia nchi jirani. Na ili kuficha asili ya madini hayo, wanabadilisha sehemu fulani ya madini hayo katika vituo vilivyopo katika nchi nyingine, kabla ya kusafirishwa nje ya nchi... Hii inalenga kuepuka vizuizi katika jukwaa la kimataifa kama vile mchakato wa Kimberly unavyofuatilia almasi za damu zinazotoka maeneo yenye migogoro.

Kwa ujumla, Wacongo hawawezi angamizwa na makundi ya waasi. Kosa lao pekee ni kuishi katika ardhi tajiri yenye rasilimali asilia. Wakati raia wa nchi hiyo wakijiandaa kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni mwaka, kiu kubwa wa wananchi ni kuona hali ya usalama inapewa kipaombele katika agenda ya uchaguzi.

TRT Afrika