Rais wa Rwanda Paul Kagame, ametoa rai kwa viongozi mbalimbali ulimwenguni kulipa “fidia halali” kwa bara la Afrika halihusiki na uzalishwaji wa hewa chafu ulimwenguni.
Kagame ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa COP29 wa kujadili mabadiliko ya hali ya hewa, jijini Baku nchini Azerbaijan.
“Tunapokutana hapa kwenye mkutano wa COP29, bara la Afrika lina nia moja tu ya kuwa mstari wa mbele kupambana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Kagame.
Hata hivyo, kulingana na kiongozi huyo wa Rwanda, malipo yatokanayo ya uchafuzi wa hali ya hewa kwa bara la Afrika, bado ni changamoto.
“Ahadi zilizotolewa kwenye mikutano ya huko nyuma bado hazijatekelezwa hadi leo. Hili halikubaliki.
“Bara letu halihusiki na uzalishwaji wa hewa chafu,” aliongeza.
TRT Afrika