Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewaachilia huru wachina 4 kati ya 17 waliokamatwa kwa tuhuma za kuendesha mgodi haramu wa dhahabu nchini humo, mamlaka ilisema siku ya Jumanne jioni.
Watu hao wanaosafiri kurejea China, walizuiliwa wiki iliyopita pamoja na wengine kutoka Congo na nchi jirani ya Burundi baada ya kushindwa kutoa stakabadhi zinazohitajika wakati wa msako mkali wa uchimbaji wa madini hayo bila kibali katika taifa hilo la Afrika ya kati.
Jean-Jacques Purusi Sadiki, gavana wa Kivu Kusini, jimbo ambalo watu hao walikamatwa, aliwaambia waandishi wa habari kwamba alishtuka kusikia habari za kuachiliwa kwao.
Wachimba migodi wa China wanadaiwa dola milioni 10 za ushuru na faini ambazo hazijalipwa kwa serikali, aliongeza.
Takriban raia 60 wa Uchina walikuwa kwenye eneo hilo na maafisa waliwaweka kizuizini 17 ambao walionekana kuwa wasimamizi.
Ubalozi wa China mjini Kinshasa haujajibu maombi ya maoni. Ubalozi wa Burundi umesema bado unasubiri maelezo kutoka kwa mwakilishi wake mjini Bukavu.
Bernard Muhindo, Waziri wa Fedha wa Kivu Kusini na Kaimu Waziri wa Madini, alisema nia ni kuboresha mfumo huo.
"Wazo si kuwatafuta watu kwa ufidhhuli, bali ni kusafisha sekta ya madini ili washirika wa kuaminika wafanye kazi ipasavyo na kisheria," aliwaambia waandishi wa habari.
Nchi hiyo ya Afrika ya kati inasema imekuwa ikijitahidi kuzuia makampuni yasiyo na leseni na wakati mwingine makundi yenye silaha kutumia akiba yake tajiri ya cobalt, cooper, dhahabu na madini mengine.