Comoro kuwachukua tena waliorejea 'kwa hiari' kutoka Mayotte baada ya mzozo wa kidiplomasia

Comoro kuwachukua tena waliorejea 'kwa hiari' kutoka Mayotte baada ya mzozo wa kidiplomasia

Comoro inasema kuwarejesha ghafla maelfu ya wahamiaji itakuwa mzigo mkubwa kwa taifa hilo.
Ufaransa na Comoro zimekuwa na safu nyingi za kidiplomasia hapo awali ambazo zilijumuisha marufuku ya visa kutoka Ufaransa / Picha: AFP / Photo: AP

Comoro imesema itaanza tena kuwakubali raia wanaorejea "kwa hiari" kutoka kisiwa jirani cha Ufaransa cha Mayotte, AFP inaripoti.

Tangazo hilo linakuja baada ya mvutano kupamba moto kati ya Comoro na Mayotte kufuatia tangazo la Ufaransa kwamba itaanza kuwafukuza maelfu ya wahamiaji haramu wa Comoro wanaoishi Mayotte.

Mwezi Aprili, Comoro, kisiwa chenye visiwa, kilicho umbali wa kilomita 238 pekee kutoka Mayotte nchi hiyo ilisema haitaweza kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji waliorejeshwa nyumbani na boti zilizo simamishwa za kutia nanga kutoka Mayotte.

Tangazo la kufukuzwa nchini lilizusha mapigano kati ya vijana na vikosi vya usalama huko Mayotte na kuchochea mvutano wa kisiasa na Comoro.

Tayari, karibu nusu ya wakazi wa Mayotte wapatao 350,000 wanakadiriwa kuwa wageni, wengi wao wakiwa ni wa Comoro.

Muungano wa Comoro unaojumuisha visiwa vitatu na Mayotte vilikuwa chini ya Ufaransa hadi mamlaka ya Comoro ilipotangaza uhuru wao kwa upande mmoja Julai 6, 1975.

Mayotte, hata hivyo, ilichagua kusalia chini ya Ufaransa hata baada ya kura ya maoni ya pili kuandaliwa mnamo 1975.

Lakini kinacho unganisha visiwa hivi ni historia. Familia zimetawanyika katika visiwa hivyo vinne, Ndoa baina ya wakazi wa visiwa hivyo zipo mara kwa mara. Pia kuna mwingiliano mkubwa wa utamaduni na biashara

Tangazo la Comoro kuchukua tena wahamiaji wanaorejea kwa "hiari" sasa linaonekana kupunguza hali ya wasiwasi. Msemaji wa serikali Houmed Msaidie aliuambia mkutano wa wanahabari kwamba mifumo ya kutambua kuondoka kwa hiari itawekwa.

Wiki iliyopita Rais Emmanuel Macron na Azali Assoumani walikutana mjini Paris ili kupunguza hali ya mvutano kati ya nchi zote mbili.

Licha ya kuwa idara masikini zaidi ya Ufaransa, Mayotte ina miundombinu na ustawi wa Ufaransa, na kuifanya kuwa kivutio cha majaribu kwa Wacomoro wanaoishi katika umaskini.

TRT World