Imetajwa kuwa chanjo ya karibu zaidi ulimwenguni kuwahi kupata chanjo dhidi ya virusi vya UKIMWI.
Utafiti umeonyesha kuwa, chanjo ya mara mbili kwa mwaka imekuwa na ufanisi wa 100% katika kuzuia maambukizo ya Ukimwi kwa wanawake, na matokeo yaliyochapishwa Jumatano yanaonyesha kuwa chanjo hiyo imekuwa na mtokeo yanayofanana kwa wanaume.
Kampuni inayotengezena chanjo, Gileadi ilisema itaruhusu matoleo ya bei nafuu na ya kawaida kuuzwa katika nchi 120 za kipato kidogo na zenye viwango vya juu vya Ukimwi, hasa katika Afrika, Kusini Mashariki mwa Asia na Karibea.
Lakini imetenga takiban eneo lote la Amerika Kusini ambapo viwango viko chini sana lakini vinaongezeka, na kuzua wasiwasi kwamba ulimwengu unakosa fursa muhimu ya kukomesha ugonjwa huo.
"Hii ni bora zaidi kuliko njia nyingine yoyote ya kuzuia tuliyo nayo, ambayo haijawahi kutokea," alisema Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS.
Aliipongeza Gileadi kwa kutengeneza dawa hiyo, lakini akasema uwezo wa dunia wa kukomesha UKIMWI unategemea matumizi yake katika nchi zilizo hatarini.
Katika ripoti iliyotolewa kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani 1 Disemba, UNAIDS ilisema kwamba idadi ya vifo vya UKIMWI mwaka jana - inakadiriwa kuwa 630,000, ilikuwa ya chini zaidi tangu kilele chake mnamo 2004, ikionyesha kuwa ulimwengu sasa uko kwenye "njia panda ya kihistoria" na ina nafasi ya kumaliza janga hilo.
Takwimu za maambukizi
Kulingana na ripoti ya UNAIDS, kati ya watu milioni 39.9 wanaoishi na virusi vya Ukimwi watu milioni 9.3 bado hawapati matibabu ya kuokoa maisha.
Ripoti inaonyesha kuwa mwaka jana, watu 630,000 walikufa kwa magonjwa yanayohusiana na Ukimwi, na watu milioni 1.3 kote ulimwenguni walipata virusi hivyo. Katika angalau nchi 28, idadi ya maambukizi mapya ya Ukimwi inaongezeka.