Al-Burhan, alisema hayo mbele kwenye kongomano la wanajeshi katika Jimbo la Mto Nile kaskazini mwa Sudan, Baraza la Utawala lilisema katika taarifa. Huku mapigano yakiendelea kati ya jeshi na kundi la RSF.
"Hakutakuwa na mazungumzo, amani, na hakuna kusitisha mapigano hadi pale kundi la RSF litakaposhindwa, ndio nchi hii inaweza kuwa na amani ," alisema Al-Burhan.
Huku mapigano makali yakiendelea kati ya jeshi na kundi la RSF katika baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na mjii mkuu wa Khartoum, Sinar, Alfasher, Aljazira.
Kundi la RSF kupitia mtandao wa "X" ilisisitiza kuendelea kwa vita hadi pale jeshi la Burhan litakaposhindwa.
Ukurasa huo ulioandikwa kwa lugha ya kiarabu na kingereza ilisema, "Kitengo cha Al-Shahama kinaingia kwenye huduma, na kufanikiwa kuangusha ndege kadhaa za jeshi huko Omdurman, na kuahidi kuwafuata wanamgambo wa Burhan kila mahali".
Mwaka mmoja sasa toka kuzuke kwa vita kati ya makundi hayo mawili, mazungumzo ya kuleta amani hayakuzaa matunda hadi sasa, huku raia wakiendela kuteseka na kulazimika kuhama makazi yao.