Spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania amewaonya wanahabari na vyombo vya habari juu ya upotoshaji wa sakata la bandari. Picha \ Tulia Akson 

Na Lulu Sanga

Spika wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Tulia Akson amethibitisha kuwa azimio la mkataba wa bandari baina ya Tanzania na Dubai bado halija afikiwa na wala kujadiliwa na bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania huku akitoa tarehe rasmi ya kujadiliwa kwa mkataba huo.

“Azimio husika kwa sasa bado lipo chini ya kamati ya pamoja kwa mujibu wa kanuni na baada ya kamati kumaliza kazi zake azimio hilo limepangwa kuingia bungeni tarehe 10 mwezi juni 2023 kwaajili ya mjadala na kupitishwa na bunge” amefafanua spika Tulia Akson

Kwa kuongezea Spika huyo wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ameonya vyombo mbali mbali vya habari nchini humo vilivyo sambaza taarifa kuwa azimio la mkataba wa bandari baina ya serikali ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai umeridhiwa.

“Taarifa zinazodai kuwa azimio hilo limesha fikiwa na bunge si za kweli, tunatoa wito kwa wanahabari kuzingatia maadili kwa kuhakikisha wanapata taarifa sahihi kutoka kwa mamlaka hususika ili kuepusha kuleta taharuki kwa jamii na uma” alisema

“Hatupendi upotoshaji na tulisha waambia milango iko wazi kama lazima gazeti kutoka piga simu kwa kiongozi akujibu usiandike taarifa ya uongo na hili ni onyo la mwisho kwa vyombo vya habari” anasisitiza Tulia Akson mbele ya mawaziri na wabunge wa Tanzania.

Tofauti na kauli ya spika huyo, mkurugenzi wa mamlaka ya bandari nchini Tanzania Plasduce Mbossa, pia amefafanua kuwa mkataba baina ya Tanzania na kampuni ya DP ya Dubai bado haujasainiwa kilicho sainiwa ni mkataba baina ya serikali hizo Dubai pekee inayoidhinisha pande hizo mbili kuanza majadiliano ndani ya miezi kumi na mbili.

“Mamlaka ya bandari bado haijasaini mkataba na kampuni yoyote. Kilicho sainiwa ni mkataba kati ya serikali mbili Tanzania na Dubai ambayo hii inaruhusu maswala ya ushirikiano na mafunzo ya tekinolojia na kuruhusu majadiliano ya awali hivyo mikataba ya utekelezaji inayoongelewa mitandaoni haipo” anasema Mbossa katika mahojiano yake na televisheni ya Taifa nchini Tanzania.

“Nimapema sana kusema atakaa miaka mingapia au atapewa eneo gani kinachoongelewa kwenye mitandao ya kijamii hakipo” anasema mkurugenzi wa mamlaka ya bandari Tanzania Plasduce Mbossa.

Tanzania ipo katika mchakato wa kuboresha bandari zake ambazo zimekuwa zikitoa huduma kwa nchi zote jirani ambazo hazina bandari kama vile DRC, Rwanda, Burundi, Zambia na mataifa mengine mengi.

Mpango wa serikali hiyo kuingia mkataba na kampuni ya DP World ya Dubai umezua gumzo kubwa ndani na nje ya nchi hiyo huku masharti ya uendeshaji na uboreshaji wa bandari hiyo yakiwa kiini cha hasira ya watanzania.

Hoja kuu mpaka sasa ni uwazi wa mikataba hiyo ambayo serikali inasisitiza kuwa bado haijaingia makubaliano yoyote ya utekelezaji yaliyo rasmi.

TRT Afrika