Ndege za kijeshi za Urusi zinaonekana katika kambi ya anga ya Hmeymim nchini Syria / Picha: Reuters

Habari za kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad zilipoenea dunia nzima, wataalamu wengi walikimbilia kuandika kuhusu uwepo wa nguvu za kijeshi wa Urusi nchini Syria.

Kambi ya jeshi la anga ya Khmeimim na kituo cha wanamaji cha Tartus —vituo pekee vya Urusi nje ya iliyokuwa Umoja wa Sovieti—inaonekana itakuwa na mwisho unaofanana na serikali iliyoondolewa madarakani.

Picha za setlaiti zikionyesha vikosi vya jeshi la Urusi wakikusanya zana zao kwa haraka katika kambi ya Khmeimim zinathibitisha utabiri huo.

Kuanguka kwa utawala wa Assad kumeishtukiza Moscow, kupelekea kubadilika kwa simulizi katika vyombo vya habari vya Urusi na majibu rasmi kutoka serikalini.

Matangazo ya Disemba 9 jioni katika chaneli ya Urusi yalielezea: "Huku mabadiliko ya utawala yakija kwa kushtukiza, kinachoshangaza zaidi ni kupooza kabisa kwa uongozi wa Syria na jeshi."

Rais Vladimir Putin yeye mwenyewe ametilia nguvu simulizi hiyo katika matangazo yake ya moja kwa moja, akisema kwamba, "Aleppo imeanguka katika mikono ya wapiganaji 350, huku wanajeshi wa serikali 30,000 na vikosi vinavyoiunga mkono serikali ya Iran vikiondoka bila kupigana."

Huku Putin akikataa fikra ya kushindwa kwa Urusi. Akisema kwamba, Moscow ilikuwa "awali imetimiza malengo yake" nchini Syria, kwa kuepusha kuanzishwa kwa "utawala wa Kiislamu" na kuwazuia magaidi kuchukua uongozi.

Muhimu zaidi, amesisitiza kwamba utawala mpya Damascus usipewe jina la magaidi, nafasi ya tahadhari ya kidiplomasia ambayo itakuwa muhimu katika majadiliano yatakayofuata.

Disemba 20, ilibainika kwamba Kanali Jenerali Nikolai Yuryev alijiuzulu kama mkuu wa kitengo cha jeshi cha ujasusi cha FSB. Katika mahojiano ya TASS ya mwaka 2018, Yuryev alielezea jukumu kuu la kikosi chake nchini Syria ni kuhakikisha usalama wa kambi za anga la vikosi vya Urusi.

Yuryev ameondoka huku kukiwa na wasiwasi kuhusu uwepo wa kijeshi la Urusi katika kanda.

Hivi sasa, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yaşar Güler anasema haoni Urusi ikijitoa moja kwa moja. Kwa mujibu wake, Urusi inakusanya zana zake za kijeshi kutoka sehemu mbalimbali za nchi na kuwekwa katika kambi mbili, kambi ya Khmeimim iliyopo Latakia na kituo cha wanamaji kilichopo Tartus.

Wakati Moscow imewaondoa baadhi ya wafanyakazi wake wa kidiplomasia, huku wanadiplomasia wa Urusi wakijadili kuondolewa moja kwa moja kwa vikosi vya Urusi, Assad mwenyewe anaripotiwa kutoroka kupitia kambi ya Khmeimim kwa msaada wa Urusi Disemba 8, baada ya utawala wake kuanguka.

Taswira tata inaibuka nyuma ya pazia.

kwa mujibu wa The Economist, majadiliano yanaendelea kati ya Urusi na Hayat Tahrir al-Sham (HTS), ambayo imekuwa na nguvu katika Syria mpya. Cha kushangaza, HTS inaonyesha utayari kuhusiana na vikosi vya Urusi kuendelea kuwepo.

"Hakuna mstari mwekundu: hii ni kutokana na maslahi, sio fikra" kimesema chanzo cha HTS kinachofahamu majadiliano hayo.

Haya yanaweza kuonekana kinyume, hasa ikizingatiwa kwamba Urusi kwa muda mrefu imekuwa ikimuunga mkono Assad.

Hata hivyo, wataalamu wanaona kuna mantiki katika hilo. Utawala mpya wa Syria unakabiliwa na kitendawili.

Wanataka kutambulika kimataifa, huku kutengwa kwa Taliban Afghanistan ikiwa ni tahadhari kwa HTS. Kuendelea kuacha kambi ya Urusi inaweza kuwa sehemu ya utambulisho wa kidiplomasia kutoka Moscow, hasa wakati ambapo nchi za Magharibi zinaonekana kutilia shaka serikali wakati ambapo HTS—ikizingatia uhusiano wake wa zamani na Al-Qaeda.

Kuendelea kwa harakati za Israel ni uhalisia mwengine. Mashambulizi ya hivi karibuni ya Israeli katika vituo vya silaha za Syria—sio kwa majibu ya mashambulizi ya HTS lakini kwa madai ya kuepusha tishio dhidi ya ardhi ya Israeli—wakati ikieleweka, inaweza kuisukuma HTS kuruhusu kuendelea kuwepo kwa kambi za Urusi kama sehemu ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya Israeli.

Uwepo wa vikundi vya kigaidi kaskazini mashariki mwa Syria kunaongeza uhalisia. Iwapo Marekani itaongeza uungaji mkono kwa magaidi wa PKK/YPG, HTS inaweza kuona uwepo wa jeshi la Urusi kama sehemu inayoweza kukabiliana na ushawishi wa Marekani katika kanda.

Urusi imejitolea misaada ya kibinadamu kubadilishana na ufikaji wa kambi, lakini utawala mpya unataka ushirikiano zaidi wa kidiplomasia na uchumi na kutambuliwa.

Wakati huo huo, Ukraine, licha ya kuwa katika vita na Urusi, tayari imetoa ngano kwa Syria.

"Tuko katika hatua ya kwanza ya majadiliano. Watu wanajaribu kuzuia umwagikaji wa damu; wangependa kujenga maisha mapya. Tunalazimika kuboresha mahusiano. Nchi imekufa. Watu maskini sana," mwakilishi wa HTS ameiambia jarida la The Economist.

Wakati huo huo, baadhi ya mawaziri wa Umoja wa Ulaya wanasisitiza Urusi iondolewe Syria.

Mwakilishi wa EU wa masuala ya Mambo ya Nje Kaja Kallas amesema suala hilo litajadiliwa katika mazungumzo na uongozi mpya wa Syria.

Hata hivyo, uhalisia unaweza kuwa tofauti na matarajio ya wanadiplosia wanavyotarajia.

Kwa Urusi, kudumisha kambi zake nchini Syria kuna umuhimu wa kimkakati. Kambi ya Khmeimim ina jukumu muhimu katika kuunga mkono uwepo wa Urusi barani Afrika, wakati kituo cha majini cha Tartus kinahakikisha uwepo wa Mediterania, muhimu sana ikizingatiwa ufikiaji wa mipaka kupitia Bahari Nyeusi kwa sababu ya vikwazo vya Mkataba wa Montreux juu ya kupita kwa meli ya kijeshi.

Kwa hivyo, licha ya kuenea kwa hisia za kupinga Urusi kati ya Wasyria waliochoshwa na vita, mamlaka mpya inaonekana tayari kwa njia ya kisayansi. HTS hutafuta kusawazisha vishawishi mbalimbali vya nje bila kujipanga kikamilifu na nguvu yoyote moja. Katika mchezo huu mgumu, kambi za Urusi zinaweza kudhibitisha njia muhimu ya mazungumzo katika mazungumzo juu ya mustakabali wa nchi.

Hali hiyo kwa mara nyingine inaonyesha kwamba siasa za kimataifa mara chache hutoa suluhu rahisi. Kile ambacho hapo awali kinaonekana moja kwa moja mara nyingi hujidhihirisha kama mtandao wa mapendeleo, ambapo nadharia ya vitendo mara kwa mara hupinga itikadi. Hatima ya kambi za Urusi nchini Syria zinaweza kuwa mfano wa kushangaza wa kanuni hii.

TRT Afrika