Arobieke: ‘Ninapenda kuonyesha maisha ya kipekee ya Kiafrika katika michoro yangu’

Arobieke: ‘Ninapenda kuonyesha maisha ya kipekee ya Kiafrika katika michoro yangu’

Sanaa ya picha ya Tomiwa Arobieke inapata mskumo kupitia urithi wake wa Kiyoruba na tamaduni nyingine za Kiafrika.
Mitindo ya nywele inayofanana na taji katika sanaa ya Tomiwa Arobieke inazungumzia historia na tamaduni za utawala. /Picha: Tomiwa

Na Pauline Odhiambo

Mambo matatu yanajitokeza katika usanii wa Tomiwa Arobieke - mitindo ya nywele ya Kiafrika ya kipekee, muundo wa maua maridadi na ngozi ya kahawia iliyokolea.

Msanii huyo wa Nigeria anavutiwa na urithi wake wa Kiyoruba na tamaduni mbalimbali za Kiafrika ambazo zinaonyesha uzuri wa mitindo ya kiasili.

"Ninapenda kuonyesha maisha ya kipekee ya Kiafrika katika michoro yangu ambayo inafichua njia yetu ya kuvaa na mitindo tofauti ya nywele tunayochagua," msanii huyo wa picha anaiambia TRT Afrika.

Sanaa ya picha inaonyehsa aina ya sanaa ya kisasa ambayo huhifadhi hali halisi ya ulimwengu na umbo la mwanadamu.

Kulingana na jukwaa la Clarendon Fine Art, aina hii inajumuisha picha zinazoonyesha vitu na matukio pamoja na mchoro.

Sanaa ya Tomiwa inajivunia aina za kipekee za mitindo ya Kiafrika. Picha: Tomiwa

Tamaduni za kifalme

Mojawapo ya kazi ya hivi punde ya Tomiwa ni ‘Goddess’ - picha iliyopewa jina linalostahili ya msichana Mwafrika aliyevalia staili ya kipekee ya Kiafrika.

Mtazamo wake wa kujiamini na hali ya utulivu inayolingana na rangi nzuri za vazi lake.

"Ninapendelea kuchora umbo la mwanamke kwa sababu zinaleta uzuri wa utamaduni wa Kiafrika vizuri," mchoraji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaelezea.

Michoro yake ya kike katika takriban picha zake zote zina mitindo ya nywele ya kina - iliyofumwa kwa njia ya ajabu ambazo muundo yake inapendeza.

Athari za mchoro wake ni mwonekano unaofanana na taji unaosimulia historia na tamaduni za utawala.

Michoro yake iliyopewa jina la ‘Elegance,’ ‘African Queen’ na nyingine nyingi inajivunia mitindo ya asili ya nywele na vijenzi vya kipekee ya mitindo ya Kiafrika.

Sanaa nyingi za Tomiwa zina picha za maua zinazowakilisha uzuri wa tamaduni za Kiafrika. Picha: Tomiwa

Picha za wanandoa

"Pia ninafurahia kuchora wanandoa kwa sababu ninaona fikra ya mapenzi katika mazingira ya Kiafrika kuwa ya kuvutia sana," asema mzaliwa huyo wa jimbo la Ondo.

Mchoro wake ulioitwa 'Companion' uliochorwa mnamo 2022 ulikuwa moja ya kazi yake ya kwanza inayojumuisha wanandoa.

Amechora picha nyingi zinazofanana tangu kazi hio ya kwanza, akiongeza vijenzi vya asili ili kudokeza afya njema, uzazi na uwingi.

"Kuonyesha upendo kati ya wanandoa pia huongeza wazo la amani na mazingira fulani na kukuza mshikamano na asili pia," Tomiwa anasema.

"Ninapenda kuongeza picha za maua katika picha zangu nyingi ili kuwakilisha mambo mazuri ambayo yanaweza kuchanua kutokana na upendo na mahusiano ndani ya mazingira ya Kiafrika," anaongeza.

Picha za wana ndoa zibazochorwa na Tomiwa. /Picha: Tomiwa

‘Aro Meta’

Michoro ya Tomiwa unaoitwa ‘Aro Meta’ unafafanua zaidi uhusiano thabiti wa urafiki.

"Katika lugha ya Kiyoruba 'aro meta' ni neno la marafiki walio karibu sana hivi kwamba tabia zao zinafanana," aeleza.

“Marafiki kama hao sikuzote huonwa wakiwa pamoja na mara nyingi huwa na mtindo sawa wa kuvaa au kuzungumza.”

Mchoro mwengine unaofanan na huo, lililopewa jina la Tomiwa 'Men Affairs' ni la kuonyesha uhusiano wa kindugu na pia mshikamano wa kijamii kati ya wanaume.

Wanaume na wanawake walioangaziwa katika michoro ya Tomiwa wanaonekana na staili za zamani katika picha za zamani lakini kwa ufafanuzi zaidi.

Michoro ya ‘aro meta’ unafafanua uhusiano thabiti wa urafiki. Picha: Tomiwa

Kuchukua fursa

Tomiwa amekuwa na mafanikio yaliyogeuza sanaa yake.

Michoro yake imeonyeshwa katika matunzio kadhaa mashuhuri katika sehemu tofauti duniani.

Anahusisha mafanikio yake kwa mapenzi ya kazi yake na kuchagua kazi ya sanaa dhidi ya vikwazo vyote.

Msanii huyo alisoma katika chuo cha Ibadan Polytechnic ambapo alihitimu stashahada ya teknolojia ya maabara ya sayansi.

"Nilikuwa nikichora kutumia penseli wakati huo na ningefanya kazi ili watu wapate pesa," msanii huyo mchanga anakumbuka.

Picha nyingi za Tomiwa zinauzwa kabla ya kuzikamilisha. /Picha: Tomiwa

Kushughulika na sanaa

Baada ya kuhitimu alifanya kazi kwa muda mfupi kama msaidizi katika taasisi ndogo ya benki kabla ya kuamua kuzingatia kikamilifu sanaa yake.

"Kutokana na kazi hiyo, niliweza kuweka pesa za kutosha kununua vifaa vya sanaa," asema. "Lakini ilichukua muda mrefu kabla ya hatimaye kuuza picha yangu ya kwanza."

Picha nyingi za Tomiwa sasa zinauzwa kabla hata hajazikamilisha.

Mchoro wake wa 'Goddess' ndio wa hivi punde zaidi kuuzwa kabla ya kukamilika.

Ushauri wake kwa wasanii wanaotarajiwa: "Sanaa inahitaji uvumilivu, kwa hivyo endelea kuifanya. Unaweza kuanza polepole lakini mwishowe utaimarika.”

TRT Afrika