Kutoka ukingoni, juu ya kuelewa kiwewe na kuhimiza watu kutafuta usaidizi wanapoumizwa na tukio la zamani. / Picha: EAI Nigeria

Na

Mazhun Idris

Katika maisha, na vile vile katika sanaa, mwandishi wa riwaya wa Kirusi wa karne ya 19, Fyodor Dostoevsky hakuwa mbali na hali ya kiwewe.

"Maumivu na mateso daima hayaepukiki kwa kutumia akili nyingi na moyo mzito," angeweza kusema, akitafakari juu ya misiba mingi ya kibinafsi ambayo alivumilia katika maisha yake yote.

Kulingana na nadharia moja, Dostoyevsky, ambaye alikufa mnamo 1881, alizungumza kwa ufahamu juu ya "kiwewe" kupitia hadithi na insha zake muda mrefu kabla ya saikolojia kuibuka kama taaluma ya kisayansi huko Uropa karibu 1879.

Karibu karne moja na nusu baadaye, kiwewe kinakubalika ulimwenguni kote kama hali inayohitaji uponyaji kisaikolojia.

Katika baadhi ya jamii zilizoathiriwa na migogoro kaskazini mwa Nigeria, filamu kuhusu athari za kiwewe inatumiwa kusaidia jamii kupambana na unyanyapaa ambao bado unahusishwa na watu waliopatwa na kiwewe wanaotafuta msaada.

Filamu inayoitwa 'From the Brink', inayohusu unyanyasaji wa kiwewe imetolewa na 'Equal Access International', shirika lisilo la faida la kimataifa linalofanya kazi ili kusaidia jamii duniani kote "kuendesha mabadiliko endelevu na yenye kuleta mabadiliko".

Wanawake na wazee walijitokeza kutazama filamu hiyo. / Picha: EAI Nigeria

"Tunatumia sinema ya kitamaduni ya jamii, kutembelea jumuia, na kuandaa vipindi vya utazamaji wa pamoja katika maeneo ya wazi ya umma," afisa mkuu wa shirika hilo, anaiambia TRT Afrika.

"Tumefanya vikao katika takriban jumuiya kumi na mbili katika majimbo matatu ya Nigeria - Plateau, Kaduna, na Kano."

Ni sawa kutafuta msaada

Muktadha wa filamu hii 'From the Brink' unalenga kufundisha mabadiliko ya kijamii na kitabia kupitia ufahamu wa hadithi.

Hadithi inasimuliwa kupitia yaliyomfika Sarah, mwanamke ambaye anayeishi na kovu la kiwewe maishani mwake, ambayo kitaalamu inaitwa "uzoefu wa utotoni".

Kama Dostoevsky, ambaye hakuwahi kupata nafuu kutokana na mshtuko wa kusubiri kuuawa hadharani huko Saint Petersburg akiwa na umri wa miaka 27 kabla ya mfalme kumsamehe, Sarah anasumbuliwa na siku za nyuma.

Ilibainika kuwa wazazi wa Sarah waliuawa mbele yake wakati wa mzozo wa kijamii.

Baada ya kupoteza familia yake, anahamia kwa shangazi yake, na kisha kudhulumiwa kingono na mume wa mwanamke huyo.

Sinema ya jamii ni chombo maarufu cha mawasiliano kinachotumiwa kubadilisha jamii. / Picha: EAI Nigeria

Sarah anaonyeshwa kuwa na kiwewe kiasi kwamba anapokua na kuamua kuolewa, ndoto zake za kutisha huwa mbaya zaidi. Ana muona mume wake na yule mnyanyasaji wa utoto kana kwama wanakuja kumuua.

Mume wake anayehuzunika na hali hio, anaamua kutafuta msaada na kumshawishi kuungana naye kuonana na mshauri wa afua. Anapuuza watu katika jamii ambao alihofia wanaweza kumwita Sarah "mwenda wazimu" kwa kutafuta msaada kwa afya yake ya akili.

Sarah na mume wake wanapata matibabu kwa mshauri wa afya, huku watazamija wakifurahia hilo, waliishi kwa furaha milele.

"Sarah ni mfano wa mtu anayepambana na majeraha mengi, na kusababisha kujitenga na hata wale wanaotaka kumsaidia - katika kesi hii, mume wake anayeelewa hali yake," afisa huyo anasema.

Kupambana na hali ya kiwewe ni ngumu

Kiwewe ni hali ya uzoefu mwingi ambayo watu hupitia, lakini hawawezi kushughulikia peke yao.

Muktadha wa filamu unalenga kufundisha mabadiliko ya kijamii na kitabia kupitia ufahamu  wa hadithi. / Picha: EAI Nigeria

Kiwewe kinaweza kutokana na unyanyasaji wa nyumbani, unyanyasaji wa kijinsia, na changamoto zingine za afya ya akili. Inapoanza kuathiri mwingiliano wa mwathiriwa na watu, mtu huyo anaweza kutenda hivi kwa ukali.

Wataalamu wanasema kiwewe hakipaswi kulinganishwa na "wazimu". Wala kusiwe na aibu au mwiko wowote kuhusu kutafuta msaada.

Kama unyogovu, mara nyingi, uponyaji kutoka kwa kiwewe huanza wakati unaweza kuzungumzia shida yako. Kuna maelezo ya kimatibabu kuhusu jinsi kushinda kiwewe kunachangia amani na ustawi wa binadamu.

Ujumbe wa filamu ya 'From the Brink' unahusu kuelewa kiwewe na kuwatia moyo watu kutafuta usaidizi wanapoumizwa na tukio la zamani.

"Tulifanya maonyesho ya sinema katika maeneo ya serikali za mitaa ya Nasarawa, Ungogo na Gezawa katika Jimbo la Kano", anasema afisa wa shirika la Equal Access International, ambaye pia anaongoza mpango wa kutoa onyo wa mapema na suluhu ya mapema kwa ambao wanakabiliana na migogoro ya vurugu katika baadhi ya majimbo ya Nigeria.

Sinema kama dawa ya maumivu

Kutoa elimu kwa kutumia sinema ni kielelezo cha ushiriki wa kijamii na kiraia ambapo mradi unapelekwa kwenye mlango wa jumuiya zinazolengwa.

"Utafiti unaonyesha kuwa jamii za kaskazini mwa Nigeria zina upendo wa kina kwa tamthilia, na njia bora za kutangaza maonyesho ya tamthilia ni redio na televisheni," shirika linasema.

Kwa sababu ya mambo kama vile upatikanaji rahisi na umuhimu wa kihistoria, redio na sinema za jamii zimekuwa zana nyingi za kampeni za umma, mawasiliano ya umma na wito wa kuchukua hatua.

Kudharau afya ya akili na kutafuta msaada dhidi ya kiwewe husaidia kupatikana kwa uponyaji. / Picha: EAI Nigeria

Baada ya kutazama filamu hiyo, waandaaji hushirikisha watazamaji ili kupata maoni kulingana na uzoefu wao na mafunzo wanayojifunza kutoka kwa filamu.

"Kipindi hiki kimepata watazamaji tofauti , kuanzia vijana, wanawake na viongozi wa kimila. Huko Barikin Ladi, jimbo la Plateau, waendesha pikipiki walisimama peke yao kutazama filamu hiyo. Jama'a katika Jimbo la Kaduna ilikuwa na onyesho mbele ya nyumba ya mkuu wa wilaya. Huko Kafanchan, chifu wa jamii aliketi kati ya wakaazi wa eneo hilo kutazama filamu hiyo," afisa huyo anaongeza.

Kuzingatia vikundi vilivyo hatarini

Mradi wa filamu ulitayarishwa mwaka wa 2024 ili kufikia watu ambao wanaonyesha dalili za kiwewe kilichosababishwa na migogoro, wale wanaoishi katika maeneo ya migogoro na kambi za waliohamishwa, na wagonjwa waliopatikana na Ugonjwa wa msongo wa mawazo baada ya tukio la Kiwewe.

Waandaaji walitambua majimbo ya Nigeria ambayo yanapambana na changamoto za kijamii na kiusalama kama vile unyanyasaji wa kijinsia, uasi wa kidini, migogoro ya wakulima na wafugaji, na mivutano ya kijamii au ya kikabila.

"Baadhi ya watu hawa wamepoteza wanafamilia au mali. Wanahitaji usaidizi wa kisaikolojia na uponyaji bila hofu ya kunyanyapaliwa," anafafanua.

Tangu kuonyeshwa kwake hadharani, filamu ya 'From the Brink', imepokea maoni chanya kutoka sehemu kadhaa.

Kulingana na watayarishaji, filamu hiyo ilirekodiwa katika mazingira mawili tofauti yenye majina tofauti ya wahusika ili kufanana na mazingira ya kitamaduni ya kaskazini mwa Nigeria.

TRT Afrika