Rais Cyril Ramaphosa: Afrika Kusini ni mwenyeji wa Mkutano wa 15 wa BRICS 2023, mjini Johannesburg / Picha: Reuters

Viongozi wa mataifa ya BRICS - Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini wamejumuika Johannesburg kwa mkutano wa kilele huku wakilenga kujadili maswali mbalimbli ikiwemo upanuzi wa wanachama huku baadhi ya wanachama wakishinikiza kuunda umoja huo katika kukabiliana na Magharibi.

Ramaphosa ni mwenyeji wa Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wanaoshiriki mkutano utakaoandaliwa kuanzia Agosti 22 hadi 24.

Harakati na dharura za kuimarisha umoja huo wa BRICS umeshika kasi kufuatia ongezeko la mvutano wa kimataifa uliochochewa na vita vya Ukraine na kuzidisha ushindani kati ya China na Marekani ambao wakati fulani umekumbwa na mgawanyiko wa ndani na ukosefu wa maono madhubuti.

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva  atua Afrika Kusini kushiriki BRICS. Picha: AFP

"BRICS pana itawakilisha kundi tofauti la mataifa yenye mifumo tofauti ya kisiasa ambayo inashiriki nia moja ya kuwa na utulivu wa kimataifa," rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, alisema katika hotuba yake kabla ya mikutano hiyo.

Kukuza matumizi ya sarafu za ndani za nchi wanachama pia ipo kwenye ajenda. Waandaaji wa mkutano wa kilele wa Afrika Kusini, hata hivyo, wanasema hakutakuwa na majadiliano ya sarafu mbadala ya BRICS, wazo lililotolewa na Brazil mapema mwaka huu kama njia mbadala ya utegemezi wa dola.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, hajawasili Afrika Kusini na badala yake atajiunga kwa njia ya kidijitali huku akisakwa chini ya hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa madai ya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Rais wa Urusi Vladimir Putin, hajafika Afrika Kusini na badala yake atajiunga kwa njia ya kidijitali. 

Kwa muda mrefu, upanuzi wa wanachama umekuwa lengo la China yenye uzito mkubwa, ambayo inatumai kuwa uanachama mpana zaidi utatoa mchango kwa kundi ambalo tayari lina asilimia 40 ya watu duniani na robo ya Pato la Taifa.

Viongozi hao watafanya tafrija ndogo na chakula cha jioni Jumanne jioni ambapo wana uwezekano wa kujadili mfumo na vigezo vya kukaribisha nchi mpya.

Lakini upanuzi umekuwa gumzo joto

Urusi ina nia ya kuleta wanachama wapya ili kukabiliana na kutengwa kwake kidiplomasia kutokana na mashambulizi yake dhidi ya Ukraine. Afrika Kusini pia imetoa sauti ya kuungwa mkono.

India, ambayo inahofia utawala wa China na imeonya dhidi ya upanuzi wa haraka, ina "nia nzuri na nia iliyo wazi", Waziri wa Mambo ya Nje Vinay Kwatra alisema Jumatatu. Brazili, wakati huo huo, ina wasiwasi kuwa kuongezeka kwa BRICS kutapunguza ushawishi wake.

Wakati uwezekano wa upanuzi wa BRICS ukiwa bado hewani, ahadi ya umoja huo wa kuwa bingwa wa "Global South" inayoendelea na kutoa njia mbadala kwa utaratibu wa dunia unaotawaliwa na mataifa tajiri ya Magharibi tayari inapata nguvu.

Zaidi ya nchi 40 zimeonyesha nia ya kujiunga na BRICS, wanasema maafisa wa Afrika Kusini. Kati yao, karibu dazeni mbili wameomba kukubaliwa rasmi.

TRT Afrika na mashirika ya habari