DRC demos

Takriban watu saba wameuawa katika machafuko katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maafisa wa eneo hilo walisema siku ya Jumamosi, baada ya watu kufanya maandamano kupinga mashambulizi makali yanayofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa Daesh.

Kwa mujibu wa vyombo vya usalama, kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) lenye mfungamano na DAESH, wanadaiwa kuwaua zaidi ya watu 40 katika shambulio katika kijiji cha Mayikengo wiki hii na zaidi ya 80 katika mashambulizi dhidi ya vijiji vingine vya jimbo hilo wiki iliyopita.

Ukosefu wa usalama umechochea ghadhabu kwa umma, na kusababisha kuuawa kwa askari wawili na dereva wao katika eneo la Lubero na umati wa watu ambao walichoma gari lao usiku wa kuamkia Ijumaa, afisa wa eneo hilo Julio Mabanga aliiambia Reuters.

''Siku ya Jumamosi, mapigano zaidi katika eneo hilo kati ya vikosi vya usalama na wakazi wa eneo hilo yalisababisha vifo vya watu wengine watatu: raia, mwanajeshi, na wakala wa idara ya upelelezi ya taifa ya ANR,'' Mabanga alisema.

Kwengineko katika mji wa Butembo, mamia ya vijana waliingia barabarani wakiwa na vijiti, wakiimba nyimbo za kukemea ukosefu wa usalama ulioenea.

''Meya wa Butembo, Mowa Baeki Telly alithibitisha kuwa raia mmoja aliuawa wakati wa mapigano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji mjini humo.

Wapiganaji waasi wa ADF wanaaminiwa kutokea nchi jirani ya Uganda, lakini sasa wamekita kambi katika eneo lenye utajiri wa madini Mashariki mwa Congo.

Baadhi ya viongozi wa magharibi kutoka nchi tajiri duniani waliokutana Italia mwishonbi mwa wiki, walizungumzia migogoro inayokumba ma eneo ya Sudan na DRC hasa kutokana na mashambulio yamakundi ya waasi kama haya.

TRT Afrika na mashirika ya habari