Wakati huohuo, katika Chuo Kikuu cha Ankara Medipol, wanachuo walipiga kambi katika uwanja wa katikati wakibeba mabango yenye kupinga mashambulizi ya Israeli na kuiunga mkono Palestina / Picha:  AA  

Kumekuwepo maandamano ya vyuo vikuu vyote nchini Uturuki kupinga mashambulizi ya Israeli katika eneo la Gaza ya Palestina.

Katika kampasi ya Chuo Kikuu cha Istanbul katika wilaya ya Avcilar siku ya Jumanne, wanafunzi walipaza kulaani shambulio la hivi majuzi kwenye kambi ya Rafah kusini mwa Gaza.

Akizungumza kwa niaba ya kundi hilo, Nurettin Ozel alishutumu mashambulizi ya mabomu dhidi ya raia wasio na hatia wanaotafuta hifadhi Rafah na kuuita "ukiukwaji mkubwa wa ubinadamu."

Katika wilaya ya Zeytinburnu, wanafunzi ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Anadolu nchini Uturuki (AGD), walikusanyika nje ya chuo kikuu cha Chuo Kikuu cha Biruni na kupinga shambulio la Rafah.

Fatih Karagul, mkuu wa tume ya Vyuo Vikuu vya AGD Istanbul, alisisitiza dhamira ya kundi hilo kwa kadhia ya Palestina na kusisitiza mshikamano na wanyonge.

Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Gaziantep walikusanyika katika mji huo wakiwa na bendera za Uturuki na Palestina kwenye mkahawa wa kati kushutumu uchokozi wa Israeli huko Rafah.

Abdulkadir Goregen, mratibu wa Taasisi ya Vijana ya Uturuki (TUGVA) alilaani uyama unaoendelezwa na Israeli dhidi ya Wapalestina.

Maandamano ya kitaaluma

Katika Chuo Kikuu cha Mus Alparslan, wasomi na wanafunzi waliandamana kupinga mashambulizi dhidi ya Palestina. Wakiongozwa na rekta na washiriki wa kitivo, walionyesha mshikamano na watu wa Gaza.

Wakati huo huo, katika Chuo Kikuu cha Ankara Medipol, wanafunzi walikusanyika katika ua wa kati na kuonyesha mabango ambayo yaliyolaani mashambulizi ya Israel na kueleza kuunga mkono kadhia ya Palestina.

Mwanafunzi wa sheria Muhammed Onur Gezgin aliangazia shambulio la hivi majuzi la Israel dhidi ya raia huko Rafah.

Katika Chuo Kikuu cha Izmir Katip Celebi, wanafunzi waliandaa safari ya baiskeli katika chuo kikuu kuipinga Israeli.

Vijana wegine waliandaa mkesha wa mshikamano kwa Gaza, wakiapa kuangazia unyama wanaofanyiwa watu wa Palestina .

Mahmut Salih Kocak, mmoja wa wanafunzi, alisisitiza dhamira ya kudumu ya waandamanaji ya kuongeza ufahamu juu ya dhuluma wanayokabiliwa Wapalestina.

Kutuhumiwa kwa mauaji ya kimbari

Israeli ilianzisha mashambulizi ya anga Jumapili kwenye kambi ya watu waliokimbia makazi yao huko Rafah na kusababisha vifo vya takriban watu 45, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Vifaru vya Israel vimeonekana katikati mwa Rafah kwa mara ya kwanza, kuashiria awamu mpya ya mashambulizi yake ya kikatili ambapo zaidi ya Wapalestina 36,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa na zaidi ya 80,000 kujeruhiwa wakati wa uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji katika Tel Aviv.

Israeli inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Uamuzi wa muda uliiamuru Tel Aviv kusitisha vitendo vya mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu inatolewa kwa raia huko Gaza.

Wakati huo huo, Norway, Uhispania na Ireland ziliitambua rasmi Palestina kama jimbo Jumanne, katika kile Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez alielezea kama "uamuzi wa kihistoria."

TRT Afrika