Wafanyakazi wa TRT wavamina Gaza | Picha: Others

Umoja wa Mataifa yasema shambulio la Israeli dhidi ya timu ya TRT Arabi ni mfano mwingine dhahiri na wazi wa hatari wanazokumbana nazo wanahabari huko Gaza, yatoa wito wa 'uchunguzi wa wazi na wa kuaminika'.

Waandishi wa habari wawili wa TRT Arabi wamejeruhiwa katika shambulio jipya la Israeli kwenye kambi ya Nuseirat huko Gaza ya Kati. Mwandishi mpiga picha Sami Shehadeh alijeruhiwa vibaya huku madaktari wakilazimika kukata mguu wake wa kulia.

Kulingana na ushuhuda wa mashahidi, jeshi la Israeli lililenga kundi la wanahabari, ikiwa ni pamoja na timu ya TRT Arabi, waliokuwa wakikusanya habari katika kambi ya wakimbizi ya Nuseirat. Baadhi ya wanahabari walijeruhiwa baada ya kupigwa na risasi za vifaru.

Mwandishi wa TRT Arabi, Sami Berhum na wanahabari wengine pia walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Kupitia maelezo ya Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Gaza, takribani wanahabari 140 wamepoteza maisha yao katika mashambulizi ya Israeli huko Gaza.

TRT World