Waandamanaji wanaounga mkono Palestina wakiwa nje ya jengo la EU, mjini Barcelona, Uhispania. /Picha: Reuters

Uhispania, Norway na Ireland zimelitambua rasmi taifa la Palestina, na kukaidi Israeli iliyolaani hatua hiyo.

Nchi hizo tatu za Ulaya zinaamini kuwa mpango wao una athari kubwa ambayo huenda ikahimiza wengine kutambua taifa la Palestina.

Hatua ya Oslo ya kulitambua taifa la Palestina imeanza kutekelezwa, Waziri wa Mambo ya Nje Espen Barth Eide alipongeza hatua hiyo kama "siku maalum kwa uhusiano wa Norway na Palestina."

"Norway imekuwa mmoja wa watetezi wa dhati wa taifa la Palestina kwa zaidi ya miaka 30," aliongeza.

Muda mfupi baadaye, Uhispania ilifuata mkondo huo, huku msemaji wa serikali Pilar Alegria akithibitisha kuwa baraza la mawaziri limeitambua rasmi taifa la Palestina, na kutimiza "siku ya kihistoria."

Hatimaye, serikali ya Ireland, nayo pia ilitangaza kuitambua rasmi taifa la Palestina.

TRT World