"Hatuwezi kuruhusu kufanya kampeni ya muda mrefu na Waziri Mkuu ambaye umma hauna imani naye." Yair Lapid amesema. / Picha: Reuters Archive

Kiongozi wa upinzani wa Israel Yair Lapid amemtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujiuzulu kwa kile alichokitaja jinsi serikali inavyoshughulikia vibaya mzozo na Palestina.

"Netanyahu anafaa kuondoka sasa wakati wa mapigano," Lapid aliiambia televisheni ya Israeli ya Channel 12.

"Serikali hii haifanyi kazi," alisema. "Tunahitaji mabadiliko-Netanyahu hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu. Hatuwezi kuruhusu kufanya kampeni ya muda mrefu na waziri mkuu ambaye umma hauna imani naye."

Lapid alibainisha kuwa chama chake, Yesh Atid, yaani 'Kuna Siku za Usoni,' kinaweza kujiunga na "serikali ya ujenzi wa kitaifa" na chama cha Likud, lakini alisisitiza kuwa "Netanyahu hawezi kuongoza."

Kulingana na kura ya maoni ya hivi karibuni, asilimia 66 ya Waisraeli wanataka uchaguzi wa mapema baada ya kumalizika kwa vita vinavyoendelea vya Israeli dhidi ya Gaza iliyozingirwa.

Vita hivyo vilianza baada ya shambulio la mpakani na kundi la Kipalestina la Hamas, mnamo Oktoba 7.

Tangu muda huo, Israeli imeendelea na shambulio lake la Gaza, na kuua angalau Wapalestina 11,500, zaidi ya nusu yao wakiwa wanawake na watoto.

Maelfu ya majengo, ikiwemo hospitali, misikiti na makanisa, pia yameharibiwa.

Tangu wakati huo, Israeli imeendelea na mashambulizi dhidi ya Gaza, ambayo yameleta maafa makubwa katika eneo hilo.

Wakati huo huo, Idadi rasmi ya Waisraeli waliokufa ni 1,200.

Baraza la Usalama la UN, lilipitisha azimio siku ya Jumatano, huku likitaka kuachiliwa mara moja kwa mateka wote walioshikiliwa na Hamas na kufunguliwa kwa njia za kibinadamu katika eneo lote ili kuokoa na kulinda maisha ya raia.

TRT World