Fidan alisema Hamas hapo awali imeonyesha mtazamo mzuri kuhusu kusitishwa kwa mapigano. Picha: AA

Akizungumza na mwenzake wa Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ameitaka Israeli kuepuka "vitendo vya uchochezi" ambavyo vinaweza kusababisha kuongezeka zaidi kwa migogoro, akielezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mvutano katika eneo hilo.

Katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, yaliyopangwa kufuatia kwa ombi la Blinken, Fidan alisisitiza haja ya kutumia shinikizo kwa Israeli kwa usitishaji wa kudumu wa Gaza, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki alisema mnamo Jumatatu.

Wakati wa mazungumzo ya simu, maafisa hao wawili walijadili mchakato wa mazungumzo kati ya Israeli na Hamas na kuongezeka kwa mvutano katika eneo hilo, alisema Oncu Keceli.

"Waziri Fidan alisema kwamba mauaji ya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas (Ismail) Haniyeh na mauaji yanayoendelea dhidi ya Wapalestina kwa mara nyingine tena yalidhihirisha kuwa Israeli haipo tayari wa mazungumzo ya amani," Keceli aliongeza.

Fidan pia alisema Hamas hapo awali imeonyesha mtazamo mzuri kuhusu kusitisha mapigano.

TRT Afrika