Jitahada zinaendelea kuongeza msimu wa utalii katika wilaya ya Dalaman na kuongeza idadi ya ndege za moja kwa moja kati ya Uingereza na eneo hilo./Picha AA

Watalii milioni nne kutoka Uingereza wanatarajiwa kutembelea Uturuki mwaka 2024, Balozi wa Uingereza nchini Uturuki amesema.

Idadi hiyo inatazamiwa kuzidi milioni 5 ifikapo mwaka 2025, alisema Jill Morris siku ya Alhamisi, wakati za ziara yake katika hoteli ya kitalii inayopatikana katika mji wa Fethiye, Kusini Magharibi mwa jimbo la Mugla.

Morris pia alipata wasaa wa kumtembelea meya wa Fethiye Alim Karaca, na kuongeza kuwa watalii wengi wa Uingereza hupendelea eneo la Mugla kwa ajili ya likizo.

Akisisitiza kuwa Fethiye ni kituo muhimu kwa ajili ya shughuli za kilimo na utalii, na kuongeza kuwa wageni wanaotembelea Fethiye, wataongeza thamani ya eneo hilo.

Ndani ya mfumo huo kati ya London na Ankara, inatarajiwa kuwa milango ya usafirishaji itafunguliwa kwa Uingereza kwa vituo muhimu vya uzalishaji wa kilimo, ikiwa ni pamoja na Fethiye katika kipindi kijacho, alisema.

Akionesha kufurahishwa na ziara ya Morris, Karaca alisema: “Picha za mji wa Fethiye zitaonekana katika maonesho ya ndani na ya kimataifa.

Kuongeza msimu wa Utalii

"Pia tutakuwa na vikao muhimu kwenye mabanda ya maonesho. Hatuna shaka kuwa huu utakuwa msimu mzuri sana kwa mwaka huu kwani manispaa yetu ina mchango mkubwa katika maendeleo ya utalii ya eneo hili,” alisema Karaca.

Pia, alibainisha kuwa zipo jitihada za kuongeza msimu wa utalii na vile vile kuongeza idadi ya ndege kati ya Uingereza na wilaya ya Dalaman.

"Kila mwaka, mji wa Fethiye hupata uwakilishi katika maonesho ya utalii ya London, maarufu kama WTM," alisema Karaca.

TRT Afrika