Rais Erdogan pia aligusia umuhimu wa kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ule wa maendeleo ya barabara wenye kuunganisha nchi za ghuba na zile za Ulaya, kuanzia bandari ya Faw nchini Iraq, ili kuongeza ustawi wa kanda./Picha: AA

Uturuki inatoa kipaumbele katika kudumisha usalama na utulivu wa Iraq, hususani baada ya yaliyojiri hivi karibuni huko Syria, kulingana na Rais Recep Tayyip Erdogan wakati alipokutana na Masrour Barzani, Waziri Mkuu wa Serikali ya Kikurdi ya nchini Iraq (IKRG).

Katika kikao kilichofanyika siku ya Jumanne katika Jumba la Rais jijini Ankara, Erdogan alisema kuwa Uturuki inatoa kipaumbele kwenye jitihada za kuzuia yale yaliyojitokeza Syria kuleta madhara zaidi katika kanda, imesema Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kwenye mtandao wa X.

Erdogan ameongeza kuwa vikundi vya kigaidi na washirika wao havina nafasi katika mustakabali wa Syria.

Mahusiano ya Uturuki na IKRG pamoja na masuala mengine ya kikanda, pia yalijadiliwa wakati wa kikao hicho.

Rais Erdogan pia aligusia umuhimu wa kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ule wa maendeleo ya barabara wenye kuunganisha nchi za ghuba na zile za Ulaya, kuanzia bandari ya Faw nchini Iraq, ili kuongeza ustawi wa kanda.

TRT Afrika