Ikiwa imetengenezwa nchini Uturuki, satelaiti ya mawasiliano aina ya Turksat 5A inaendelea kuboresha ufanisi wa urushaji matangazo, na kuifanya Uturuki kuwa moja ya nchi chache zenye kutumia teknolojia hiyo ya kisasa./Picha: AA

Ikiwa imetengenezwa nchini Uturuki, satelaiti ya mawasiliano aina ya Turksat 5A inaendelea kuboresha ufanisi wa urushaji matangazo, na kuifanya Uturuki kuwa moja ya nchi chache zenye kutumia teknolojia hiyo ya kisasa.

Kulingana na Waziri wa usafiri na miundombinu Abdulkadir Uraloglu, teknolojia hiyo imekuwa imekuwa ikifanya kazi kuanzia mwaka 2021, ikitoa ufanisi mkubwa kwenye nyanja ya mawasiliano.

“Kwa kutumia teknolojia za kisasa, takribani megahatzi 36 zimetumikana tumeona ufanisi mkubwa katika uwezo wa Turksat,” amesema Uraloglu.

Kulingana na Waziri huyo, satelaiti hiyo imeongeza ufanisi wa mawasiliano barani Ulaya, Mashariki ya Kati, Afrika na maeneo mengine.

“Turksat 5A inatoa suluhu la uhakika kwa ajili ya masoko ya kimataifa huku pia ikitumika katika usafiri wa majini,” amesema.

Maisha marefu

"Mapato makubwa yalipatikana hususani huko Saudi Arabia," Uraloglu aliongeza.

Waziri huyo pia alisisitiza kuwa kizazi hicho cha satelaiti kina uwezo wa kudumu kwa kipindi cha miaka zaidi ya miaka 35.

TRT Afrika