Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) limemkata makali kiongozi anayetambulika wa kundi la kigaidi la PKK kaskazini mwa Iraq, vyanzo vya usalama vimesema.
MIT ilifanya operesheni kali katika eneo la Sulaymaniyah ili kumzima Mehmet Seda Akman, kwa jina jengine, Bahoz Zagros, vyanzo hivyo vilisema Jumanne.
Gaidi huyo, ambaye alikuwa akipanga mashambulizi ya silaha dhidi ya Uturuki, alikuwa chini ya ufuatiliaji wa kijasusi wa Uturuki, waliofanikiwa kumuondoa katika operesheni ya uhakika.
Akman, maarufu 'Bahoz Zagros' aliyejiunga na kundi la kigaidi la PKK mnamo 2005, alikuwa kiongozi wa kundi hilo la kigaidi huko Sulaymaniyah.
"Walikatwa makali" humaanisha kuwa magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au walitekwa kupitia operesheni ya vyanzo vya usalama nchini Uturuki.
Tangu shambulio la kigaidi la PKK Ijumaa, lililowaua wanajeshi 12 kaskazini mwa Iraq, mashambulio ya anga ya Uturuki yamesambaratisha ngome kadhaa ya magaidi kaskazini mwa Iraq na Syria.
Aidha, Rais Recep Tayyip Erdogan ameapa kuwa Uturuki haitaruhusu wakuu wa ugaidi katika eneo hilo kuizuia nchi hiyo kufanikisha maazimio yake, na kwamba vita dhidi ya ugaidi vitaendelea.
Magaidi wa PKK wenye tawi Syria, linalojulikana kama YPG, mara nyingi hujificha kaskazini mwa Iraq ili kuandaa mashambulizi yanayolenga mipaka ya Uturuki.
Katika mashambulizi yake ya ugaidi ya zaidi ya miaka 35 dhidi ya Uturuki, PKK, iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU, imehusika katika vifo vya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake, na watoto wachanga.