Magaidi watatu wa Daesh wamekamatwa kupitia ushirikiano wa karibu wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) na Jeshi la Kitaifa la Syria (SNA).
Operesheni hizo zilitekelezwa kaskazini mwa Syria na vikosi vya usalama vya ndani vinavyohusishwa na SNA, kwa msaada wa upelelezi na uendeshaji kutoka MIT, katika eneo la Operesheni ya Amani, huko Syria.
Maafisa wa Uturuki waliripoti kuwa watu hao watatu walikuwa katika ngazi za usimamizi ndani ya Daesh.
Vifaa vilivyokamatwa ni pamoja na silaha 1 nyepesi ya kuzuia vifaru (M72LAW), mfyatua moja ya RPG , pikipiki 2, mabomu 5 ya kutupa kwa mkono, bunduki 5 aina ya AK-47, bastola 2 za Makarov, redio 1, vichwa 4 vya kupambana na vifaru (HEAT), vifaa 2 vya kushambulia vifaru yaani 'anti-tank warheads. - vichwa vya vita vya RPG (HE), fuze 5 za RPG, majarida na risasi nyingi.
Huku Uturuki ikiendeleza juhudi zake dhati dhidi ya makundi ya kigaidi yakiwemo Daesh, Al-Qaeda na PKK bila ya kutofautisha, Ujasusi wa Uturuki MIT imesalia imara katika mapambano yake thabiti dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria na maeneo mengine yanayolenga kulinda usalama wa nchi.
Mnamo 2013, Uturuki ilikuwa taifa la kwanza kulitangaza Daesh kuwa shirika la kigaidi
Tangu wakati huo, nchi hiyo imelengwa kwa mashambulio mara kadhaa na kundi hilo la kigaidi, huku zaidi ya watu 300 wakiuawa na mamia zaidi kujeruhiwa katika milipuko 10 ya kujitoa mhanga, mashambulizi saba ya mabomu na mashambulizi manne ya silaha.
Ili kukabiliana na hilo, Uturuki ilianzisha operesheni za kupambana na ugaidi ndani na nje ya nchi ili kuzuia mashambulizi zaidi.