Majeshi ya Ulinzi ya Uturuki yamewakata makali magaidi 19 wa PKK/YPG kaskazini mwa Iraq na Syria, Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo imetangaza.
“Mashujaa wetu wamefanikiwa kuwakata makali magaidi 15 wa PKK kaskazini mwa Iraq na 4 kutoka PKK/YPG kaskazini mwa Syria,” ilisema Wizara hiyo kupitia ukurasa wake wa X siku ya Jumanne.
Mamlaka za Uturuki hutumia neno "kukata makali" kumaanisha magaidi wamejisalimisha, wameuwawa au kukamatwa.
Katika kampeni yake ya takriban miaka 40 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na Umoja wa Ulaya, imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake na watoto, hususani wachanga.
YPG ni zao la PKK la Syria.
Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha kaskazini mwa Iraq ili kupanga mashambulizi ya kuvuka mpaka nchini Uturuki.