Shirika la kitaifa la ujasusi nchini Uturuki "limemuondoa" kiongozi wa kundi la kigaidi la PKK/YPG katika mji wa Ayn Al Arab, kaskazini ya Syria, vyanzo vya usalama vilisema.
Katika operesheni ya mpakani, shirika la kitaifa la ujasusi (MIT) "lilimwondoa" Mutlu Kacar, aliyepewa Jina a Karker Andok, mwanachama wa juu wa kikundi cha kigaidi katika wilaya ya Ayn Al Arab, vyanzo vilisema Jumatatu.
Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "neutralise" kuashiria magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.
Kacar, ambaye alijiunga na kundi hilo la kigaidi mnamo1997 na kushiriki katika shughuli za kigaidi katika mkoa wa haftanin kaskazini mwa Iraq mwaka 2009, alipata majeraha kwenye mkono na jicho lake katika mapigano na vikosi vya usalama.
Baada ya kuhudumu kama mkuu wa kambi ya Makhmur Rustem Cudi Kaskazini mwa Iraq mnamo 2013, mkoa wa Tel Rifaat Wa Syria mnamo 2015, na kama mkuu wa vikosi vya mitaa huko Tel Rifaat kwa PKK/YPG mnamo 2020, Kacar alichukua jukumu la kuwa kiongozi wa Ayn Al Arab kwa PKK/YPG mapema mwaka huu.
Mnamo, alienda Al-Malikiyah kaskazini mashariki mwa Syria.
Mwaka uliopita 2022, aliamuru shambulio la kigaidi dhidi ya msafara wa vikosi vya usalama vya Uturuki vinavyofanya kazi katika Eneo la Operesheni ya Ngao ya mto Eufrati kaskazini mwa Syria, na kusababisha kifo cha askari wawili mnamo Julai 24, 2021.
Tangu 2016, Ankara imeanzisha operesheni tatu za kupambana na ugaidi zilizofanikiwa kama vile Eufrati Shield (2016), Olive Branch (2018), Na Peace Spring (2019) katika mpaka wake kaskazini mwa Syria ili kuzuia kuundwa kwa ukanda wa ugaidi na kuwezesha makazi ya amani ya wakazi.
Operesheni "iliyompunguza" Kacar, ambaye kwa muda mrefu alikuwa chini ya ufuatiliaji na vikosi vya usalama, ilijiri baada ya MIT kubainisha eneo lake nchini Syria.
Katika kampeni yake ya ugaidi ya zaidi ya miaka 35 dhidi ya Uturuki, PKK, iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU — imesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000, wakiwemo wanawake, watoto, na watoto wachanga.
YPG ni tawi lake nchini Syria.