Makumi ya maelfu ya watu wanaandamana kwa mshikamano na Wapalestina katika "Mkutano Mkuu wa Palestina" mjini Istanbul mnamo Oktoba 28, 2023. / Picha: AA

Wanadiplomasia wa Israel nchini Uturuki tayari walikuwa wameondoka siku chache zilizopita, chanzo cha kidiplomasia cha Uturuki kilisema baada ya matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen juu ya kuondoka kwa wanadiplomasia wa Israel Uturuki.

"Wanadiplomasia wa Israel hawako Uturuki kwa sasa. Kufikia Oktoba 19, walikuwa tayari wameondoka nchini mwetu, " vyanzo vilibaini, na kuongeza kuwa katika barua iliyotumwa mnamo Oktoba 18 kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, wanadiplomasia katika ubalozi walikuwa wamewajulisha maafisa kwamba kwa sababu ya maendeleo ya hivi karibuni, wataondoka nchini mnamo Oktoba 19.

"Ni vigumu kufahamu Cohen aliwaamuru kina nani kurudi. Kwa sababu wanadiplomasia aliowataja katika taarifa yake walikuwa tayari wameondoka nchini mwetu," vyanzo vilisema.

Ripoti za hivi karibuni za vyombo vya habari, zikinukuu vyanzo vya Israeli, zilionyesha kuwa wanadiplomasia wa Israeli, pamoja na balozi Irit Lillian, waliondoka Uturuki kwa sababu ya wasiwasi wa usalama na sio mgogoro wa kidiplomasia.

"Kwa kuzingatia matamshi makali kutoka Uturuki, nimeamuru kurudi kwa wawakilishi wa kidiplomasia walioko huko ili kufanya tathmini mpya ya uhusiano kati ya Israeli na Uturuki," Cohen aliandika Kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Taarifa ya waziri huyo kwenye mitandao ya kijamii ilitolewa muda mfupi baada ya hotuba ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika "Mkutano Mkuu wa Palestina" mkutano wa kuunga mkono Palestina mjini Istanbul.

TRT World