Viongozi wa G20 waliokusanyika katika mji mkuu wa India New Delhi kwa ajili ya mkutano wa kilele wameshukuru juhudi za uturuki kwenye mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi, kulingana na tamko la pamoja.
"Tunashukuru juhudi za Uturuki na Mikataba ya Istanbul iliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa inayojumuisha Mkataba wa Maelewano kati ya Shirikisho la Urusi na Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa juu ya Kukuza Bidhaa za Chakula na Mbolea za Kirusi kwenye Masoko ya Dunia na Mpango wa Usafirishaji Salama wa Nafaka. na Vyakula kutoka Bandari za Kiukreni (Mpango wa Bahari Nyeusi)," tamko la New Delhi lilisoma.
Viongozi hao pia walitoa wito wa kutekelezwa "kamili, kwa wakati na kwa ufanisi" wa mpango huo ili kuhakikisha uwasilishaji "wa haraka na usiozuiliwa" wa nafaka, vyakula, na mbolea/pembejeo kutoka Urusi na Ukraine.
"Hii ni muhimu ili kukidhi mahitaji katika nchi zinazoendelea na zenye maendeleo duni, hasa zile za Afrika," iliongeza.
Malalamiko ya Urusi
Viongozi wa G20, ukiondoa Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa China Xi Jinping, walikusanyika kwa mkutano wa siku mbili ili kubadilishana mawazo kuhusu biashara, hali ya hewa na matatizo mengine ya kimataifa.
Mnamo Julai 17, Urusi ilisitisha ushiriki wake katika mapatano hayo, yaliyosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa kuanza tena mauzo ya nafaka kutoka bandari tatu za Bahari Nyeusi za Ukraine ambazo zilisitishwa baada ya "operesheni maalum ya kijeshi" ya Moscow mnamo Februari 2022.
Urusi imelalamika mara kwa mara kwamba nchi za Magharibi hazijatimiza wajibu wake, na kuna vikwazo juu ya malipo, vifaa na bima juu ya usafirishaji wa chakula chake na mauzo ya mbolea.
Uturuki inasema mpango huo unapaswa kuanzishwa tena kwa kushughulikia kasoro kadhaa ambazo zimetambuliwa, na kwamba hakuna mbadala wa makubaliano yaliyotiwa saini mnamo Julai 2022.