Vikosi vya usalama vya Uturuki vimewakata makali wanachama 12 zaidi wa kundi la kigaidi la PKK/YPG kaskazini magharibi mwa Syria, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya Uturuki ilisema.
"Magaidi kumi na wawili wa PKK/YPG, ambao walifyatua risasi za uchokozi kwenye eneo la oparesheni ya Euphrates Shield, walidhibitiwa katika operesheni iliyofaulu," ilisema taarifa ya wizara hiyo Jumapili.
Mamlaka ya Uturuki yanatumia neno "kukatwa makali" kumaanisha kwamba magaidi husika walijisalimisha au waliuawa au kutekwa.
Magaidi wa PKK/YPG wamejificha kaskazini mwa Syria, karibu na mpaka wa Uturuki, ambako wanapanga na kutekeleza mashambulizi dhidi ya wenyeji na makazi ya jirani ya Uturuki.
Tangu 2016, Ankara imezindua oparesheni tatu zenye mafanikio za kupambana na ugaidi katika mpaka wake kaskazini mwa Syria ili kuzuia uundaji wa ukanda wa ugaidi na kuwezesha makazi ya amani ya wakaazi: Euphrates Shield (2016), Olive Branch (2018) na Peace Spring (2019).
Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 40 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Uingereza, Marekani, na Umoja wa Ulaya - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto. YPG ni tawi lake la Syria.