Uturuki imetangaza kuwa itatuma treni inayojaa misaada zaidi ya kibinadamu kusaidia watu walioathiriwa na tetemeko la Ardhi katika mkoa wa Herat nchini Afghanistan.
Katika taarifa yake Jumanne, Usimamizi wa Idara ya Majanga na Dharura (AFAD) ilisema, misaada itakayopelekwa Afghanistan ni pamoja na tani 39 za blanketi, tani 8 za vitanda, tani 85 za mahema, tani 40 za vifaa vya usafi, tani 33 za nguo, tani 15 za jenereta, tani 240 za chakula, tani 30 za vifaa vya jikoni, kilo 400 za vyoo vya kubebeka, na tani 18 za hita.
Mwezi uliopita, matetemeko ya ardhi yalifululiza katika Jimbo la Herat nchini Afghanistan, lililoko kwenye mpaka na Iran, yalisababisha vifo vya takriban watu 2,500, na kulazimisha mamlaka ya Afghanistan kutoa ombi la misaada ya kimataifa.
Hapo awali, Ankara ilituma ndege mbili kutoka Wizara ya Ulinzi wa Kitaifa, ikibeba wafanyakazi wa uokoaji na misaada ya kibinadamu kufika mkoa huo.
Zaidi ya matetemeko 10 ya ardhi, makubwa zaidi kati ya hayo yaliyokuwa ya ukubwa wa 6.3, yalisababisha uharibifu mkubwa katika vijiji 16 vilivyoko katika wilaya ya Zindajan, Herat.