Uturuki yashambulia maeneo ya PKK kaskazini mwa Iraq, 'yawakata makali ' magaidi 4

Uturuki yashambulia maeneo ya PKK kaskazini mwa Iraq, 'yawakata makali ' magaidi 4

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha kaskazini mwa Iraq na Syria kupanga njama za kuvuka mpaka huko Uturuki.
Magaidi hao walilengwa katika eneo la Gara./ Picha: AA

Uturuki "imewakata makali " magaidi wanne wa PKK kaskazini mwa Iraq, karibu na mpaka wa Uturuki, Wizara ya Ulinzi ya Kitaifa ya Uturuki imetangaza.

Magaidi hao walilengwa katika eneo la Gara, taarifa ya wizara ilisema Jumapili.

Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "kuwakata makali" kumaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha kaskazini mwa Iraq na Syria kupanga njama za kuvuka mpaka huko Uturuki.

Operesheni Claw-Lock ilianzishwa mnamo Aprili 2022, ikilenga maficho ya PKK katika maeneo ya Metina, Zap, na Avasin-Basyan kaskazini mwa Iraq, karibu na mpaka wa Uturuki.

Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, Uingereza na EU - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake, na watoto.

TRT World