Fahrettin Altun amesifu uhusiano kati ya Uturuki na Libya, akisema nchi yake ina uhusiano wa kihistoria na kitamaduni na nchi ya kindugu. / Picha: AA

Uturuki itaendelea kusimama na ndugu zetu wa Libya bila kusita, kuponya majeraha yao na kuwasaidia katika kipindi kijacho, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki Fahrettin Altun amesema.

Akizungumza katika mkutano wa "Tripoli Communication Forum," Altun ameongeza kuwa nchi yake ina uhusiano wa kihistoria na kitamaduni na rafiki yetu na nchi ndugu ya Libya.

"Katika muktadha huu, mwaka uliopita, tulisaini mkataba wa makubaliano kufanikisha ushirikiano wa vyombo vya habari na mawasiliano na Libya, na kuimarisha zaidi uhusiano wetu katika sekta hiyo," alisema.

"Kujua kuwa serikali ya Makubaliano ya Kitaifa ya Libya imeipa kipaumbele "mawasiliano ya majanga na migogoro," haswa wakati wa mkutano wa jukwaa la la mawasiliano la Tripoli, inaturidhisha pia kwa niaba ya raia wa Libya.”

"Kama Uturuki, tutaendelea kufanya kazi kufanikisha ubunifu wa jamii yenye nguvu zaidi na ya kudumu, kitaifa na kimataifa, dhidi ya majanga ya asili na migogoro mengine ya kibinadamu," Altun aliongeza.

Uhusiano wa Uturuki na Libya

Ndani ya miaka ya hivi karibuni, Uturuki na Libya zimechukua hatua kadhaa kuimarisha uhusiano wao wa kihistoria, kijiografia, kisiasa, kijeshi, kiuchumi, na kitamaduni.

Kufuatia mwisho wa makubaliano ya baharini mnamo Novemba 2019, uliofafanua upya maji yao ya eneo katika bahari ya Mediterania, mataifa hayo mawili yamepanua ushirikiano wao katika utafutaji wa mafuta na gesi asilia.

Mbali na hayo, Ankara na Tripoli zilitia saini mkataba wa makubaliano ya utafutaji wa haidrokaboni katika Mashariki mwa Mediterania mnamo Oktoba 2022.

Mkataba huo unakusudia kuhifadhi haki na maslahi ya Uturuki na Libya katika maji ya mashariki ya Mediterania.

TRT World