Wizara hiyo imeoneshwa kusikitishwa na imelaani vikali shambulio hilo, na kusisitiza kuwa Uturuki itaendelea kuiunga mkono Somalia katika jitihada zake za kupambana na ugaidi./ Picha: AA  

Uturuki imesikitishwa na kulaani vikali shambulizi la kigaidi huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, ambalo liligharimu maisha ya makumi ya watu.

"Tumesikitishwa sana na vifo vya watu wengi na majeruhi kufuatia tukio la kigaidi mjini Mogadishu," ilisema Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki katika taarifa yake siku ya Jumamosi.

Takribani watu 32 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililotokea katika fukwe maarufu ya mjini Mogadishu.

Kulitokea mlipuko mkubwa na milio ya risasi katika fukwe ya Lido, siku ya Ijumaa.

Al-Shabab wakiri kuhusika

"Hatua za haraka za vikosi vya usalama ziliwadhibiti washambuliaji, wakati timu za matibabu zikiwahudumia waathirika wa tukio hilo katika la tukio," Shirika la Habari la Kitaifa la Somalia liliripoti.

Kituo cha Televisheni ya taifa ya Somalia kilitoa taarifa kama hizo lakini hakikutoa taarifa zaidi kuhusu idadi ya vifo.

Eneo hilo ni maarufu sana kwa raia, maafisa wa usalama na wafanyabiashara.

Kikundi cha Al Qaeda kimedai kuhusika na tukio hilo.

TRT Afrika