Wizara ilikariri wito wa Uturuki wa kusitisha mapigano mara moja, bila masharti na kudumu huko Gaza. / Picha: Jalada la AA

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imelaani shambulizi la Israel dhidi ya shule ya Umoja wa Mataifa ya Al Fakhoura katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia kaskazini mwa Palestina Ukanda wa Gaza.

"Tunalaani vikali shambulio la Israel dhidi ya shule ya Al Fakhoura inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa huko Gaza mnamo Novemba 18, ambalo lilisababisha mauaji ya makumi ya watoto wa Kipalestina wasio na hatia," wizara hiyo ilisema katika taarifa mapema Jumapili.

Ilisema shambulio hilo ni ushahidi zaidi kwamba Israeli "kwa makusudi na bila huruma" inalenga raia, haswa watoto, huko Gaza.

Idadi ya wanawake na watoto ambao wameuawa mikononi mwa Israel huko Gaza katika wiki tano zilizopita ni "chanzo cha aibu kwa ubinadamu," iliongeza.

Jumuiya ya kimataifa haipaswi tena "kufumbia macho Israel inayohujumu sheria na maadili yote ya kibinadamu kwa uhalifu mkubwa iliofanya," ilisema wizara hiyo

"Wale waliohusika na mauaji haya, ambayo tayari yameacha doa la giza kwenye historia ya mwanadamu, bila shaka watawajibishwa kwa maumivu yasiyoelezeka waliyosababisha."

Zaidi ya Wapalestina 12,000 waliuawa

Ikirejelea wito wa Uturuki wa kusitisha mapigano mara moja, bila masharti na kudumu huko Gaza, wizara hiyo ilitoa wito kwa "kila mwanachama mwadilifu wa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua zinazohitajika katika mwelekeo huu."

Makumi ya watu waliuawa na kujeruhiwa siku ya Jumamosi katika shambulio la Israel katika kituo cha mafunzo kinachosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika kambi ya wakimbizi.

Israel ilifanya mashambulizi ya anga na baadaye kuvamia ardhini baada ya shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la wapiganaji wa Palestina, Hamas.

Mashambulizi ya Israel tangu wakati huo yameua zaidi ya watu 12,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, yalisambatisha maelfu ya majengo ya kiraia, na kutekeleza kizuizi kamili na kusababisha uhaba wa vifaa vya msingi kama vile chakula, mafuta na dawa.

TRT World