Uturuki yafanya juhudi kuhifadhi ndege wake wakiwemo korongo / Photo: AP

Ankara

Idara ya uhifadhi wa mali asili na misitu ya kitaifa, iliyopo chini ya wizara ya kilimo na misitu, inafanya utafiti muafaka wa uhifadhi wa ndege ikiwemo kuwavisha pete za mguuni, kutia alama, kuwahesabu na kuwatia vifaa vya kuhifadhi na kutuma data za ndege hao.

Kulingana na maelezo kutoka wizara hiyo, nji nyingi hutumiwa kuwalinda na kuwafuatilia ndege hao.

Kuwavisha pete, kutia alama, na kuwawekea vifaa vya kukusanya data pamoja na kuwatazama moja kwa moja na kuwahesabu kunatoa maelezo muhimu sana juu ya tabia za ndege hao na uhamiaji wao.

Vituo vinne vya uhifadhi wa ndege nchini Uturuki, ikiwemo , Cernek iliyoko mkoa wa Bahari Nyeusi wa Samsun, Aras iliyoko mkoa wa mashariki wa Igdir, Eymir iliyoko mji mkuu Ankara, na Bogazkent iliyoko mkoa wa Mediterenia wa Antalya, vimeendelea kufanya kazi vyema.

Mwaka uliopita, kufuatia utafiti uliofanywa kote nchini, zaidi ya ndege, 28,380 kutoka aina 200 waliweza kuvishwa pete za miguu.

Watafiti wa Uturuki mwaka jana waliweza kupokea maelezo-rejeshi kutoka kwa ndege 35 wa aina 15 mbali mbali.

Maelezo ya awali zaidi yalinakiliwa baada ya ndege wa kipekee aina ya Shakwe, mwenye mgongo mweusi, ambaye alivishwa pete nchini Finland mwaka 2012 alipo onekana nchini Uturuki akiwa hai, takriban kilomita 2,809 kutoka sehemu alipo nakiliwa mwanzo mwaka jana.

Maelezo-rejeshi yalikusanywa kutoka kwa ndege 39 wa aina 13 tofauti mwaka 2021 na ndege 30 wa aina 15 tofauti na mwaka 2020.

Katika utafiti wao wanasayansi waliweka vinasa-data kwa aina tatu za tai na korongo wawili mwaka 2019.

Tai mmoja wmwenye asili iliyo changanya ya Ulaya na Asia aliwekewa mwaka 2021 na mwingine pia mwaka 2020. Korongo wanne na tai mmoja waliwekewa mwaka 2021 na huku korongo na tai wengine tena wakiwekewa mwaka jana.

Pia ndege wa majini wanahesabiwa kila mwaka katika maeneo ya chemi chemi katika uchunguzi unaofanywa wakati wa msimu wa baridi.

Utafiti huu hufanywa kati ya tarehe 15 Januari na 15 Februari kila mwaka, katika maeneo muhimu ya ndege wa majini.

AA