Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan atafika mji wa Sochi, pwani ya Urusi "hivi karibuni," kwa mujibu wa afisa wa Uturuki amesema.
"Kufikia sasa, rais wetu ametekeleza mpango huo kwa usikivu wa hali ya juu zaidi wa kidiplomasia ili kuzuia dunia isikumbwe na tatizo la chakula. Atakuwa na ziara Sochi hivi karibuni," Omer Celik, msemaji wa Chama cha Haki na Maendeleo (AK) , alisema katika mji mkuu wa Ankara.
Celik ameongeza kuwa kuna uwezenako wa kuwa na maendeleo mapya kuhusu mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi.
Hivi sasa, Uturuki inaendelea na juhudi zake za kufufua mpango wa nafaka wa Bahari Nyeusi, na inasema kuwa hakuna njia mbadala ya mpango huo.
Aidha, Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Hakan Fidan pia anatarajiwa kuzuru Urusi hivi karibuni ili kufanya mazungumzo ya ana kwa ana ili kurejesha makubaliano hayo.
Mnamo Julai 17, Urusi ilisitisha ushiriki wake katika mkataba wa nafaka wa Bahari Nyeusi, ulioongozwa na Uturuki ikishirikian na UN ili kuanza tena mauzo ya nafaka kutoka bandari tatu za Bahari Nyeusi za Ukraine ambazo zilisitishwa baada ya vita vya Urusi na Ukraine vilivyozuka Februari 2022.
Moscow imekuwa ikilalamika mara kwa mara kuwa nchi za Magharibi hazijatimiza wajibu wake kuhusu mauzo ya nafaka ya Urusi yenyewe. Inasema vikwazo vya malipo, vifaa na bima vimelemaza usafirishaji wake.