Kufuatia milipuko mikali nchini Lebanon, afisa wa wizara ya ulinzi ya Uturuki alitangaza siku ya Alhamisi kwamba Uturuki inatathmini upya hatua zake za kupata vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa na vikosi vyake vya jeshi. / Picha: AA

Uturuki inachukua hatua za kugaua na kuhakikisha usalama wa vifaa vya mawasiliano vinavyotumiwa na vikosi vyake vya jeshi baada ya milipuko mabaya huko Lebanon, afisa wa wizara ya ulinzi ya Uturuki alisema Alhamisi.

Redio zinazoshikiliwa kwa mkono zinazotumiwa na kundi lenye silaha la Hezbollah zililipuka siku ya Jumatano kote kusini mwa Lebanon katika siku mbaya zaidi ya nchi hiyo tangu mapigano kati ya kundi hilo na Israeli yalipozuka karibu mwaka mmoja uliopita, na kuzua hali ya wasiwasi baada ya milipuko kama hiyo ya vifaa vya mawasiliano 'pager' vya wanamgambo hao siku moja kabla.

Milipuko hiyo ilionekana kuleta mkanganyiko kati ya Hezbollah, wakala wenye nguvu zaidi wa Iran katika Mashariki ya Kati, na ilitokea huku mashambulizi ya miezi 11 ya Israeli dhidi ua Gaza huko Palestina, na kuzidisha hofu ya kuongezeka kwa vita katika eneo hilo.

Wanajeshi wa Uturuki hutumia vifaa vinavyotengenezwa nchini pekee lakini Ankara ilikuwa na mifumo ya ziada ya udhibiti ikiwa mtu wa tatu anahusika katika ununuzi au utengenezaji wa vifaa, afisa huyo wa Uturuki alibainisha.

"Iwe katika oparesheni tunazofanya, vita vinavyoendelea nchini Ukraine, na kama ilivyo kwa mfano wa Lebanon, hatua zinapitiwa upya na hatua mpya zinaendelezwa kama sehemu ya mafunzo tunayojifunza kufuatia kila jambo," afisa huyo alisema.

"Kuhusu suala la tukio hili, sisi kama Wizara ya Ulinzi tunafanya ukaguzi muhimu," mtu huyo aliongeza, bila kutoa maelezo zaidi.

Katika milipuko ya Jumanne, vyanzo vilisema majasusi wa Israeli walilipua kwa mbali vilipuzi viliomo katika vifaa vya mawasiliano 5000 vilivyonunuliwa na Hezbollah kabla ya kuingia nchini.

Mashambulizi hayo ambayo hayajawahi kushuhudiwa yamezua wasiwasi juu ya usalama wa mtandao katika eneo hilo.

Baraza la usalama la taifa la Iraq lilisema Jumatano kwamba litachukua hatua za kuzuia dhidi ya ukiukaji wowote unaowezekana kutoka kwa bidhaa za kielektroniki, na kuongeza kuwa ukaguzi mkali wa usalama utatekelezwa kwenye uagizaji wa bidhaa pamoja na ukaguzi wa nguvu zaidi wa mpakani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan siku ya Alhamisi aliliambia shirika la habari la Anadolu kwamba kuanzishwa kwa wakala huru wa usalama wa mtandao mahsusi kulikuwa kwenye ajenda ya serikali baada ya Rais Recep Tayyip Erdogan kueleza umuhimu wake, na kuongeza kuwa litaundwa "hivi karibuni sana".

TRT Afrika