Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa Palestina na masuala mengine muhimu ya kikanda wakati wa mkutano wa kilele mjini Cairo. / Picha: AA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amesema kuwa ulimwengu wa Kiislamu utafanya "chochote kinachohitajika" kulinda "hadhi ya Kiislamu" ya Msikiti wa al-Aqsa, mojawapo ya maeneo takatifu zaidi kwa Waislamu.

"Ulimwengu wa Kiislamu utafanya lolote linalohitajika ili kuhifadhi hadhi ya Kiislamu ya 'Haram al Sharif' kwa moyo huohuo," Fidan alisema Jumanne wakati wa hotuba yake katika mkutano wa 162 wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu.

"Tutaendelea na hatua yetu ya pamoja kuweka shinikizo kwa jumuiya ya kimataifa kukataa vitendo vya Israel."

Haram al Sharif pia inajulikana kama Msikiti wa al Aqsa, ambao umeshuhudia uvamizi kadhaa kutoka kwa viongozi wa mrengo wa kulia wa Israeli katika miezi ya hivi karibuni.

Fidan alionya wale wanaomuunga mkono Waziri Mkuu wa Israeli Netanyahu, akisema kuwa wao ni washirika wa mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayoendelea Gaza.

"Pia watawajibishwa."

Siku ya Jumatatu, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan pia aliwataka viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kufanya mkutano katika ngazi ya viongozi "bila kuchelewa zaidi" kusaidia kulinda Jerusalem dhidi ya mashambulizi yanayoendelea ya Israeli.

Kuimarisha mahusiano

Uhusiano wa Uturuki na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu umebadilika kwa kiasi kikubwa tangu kuanzishwa kwake rasmi mwaka 2003, ukiwa na hatua kadhaa muhimu.

Tukio muhimu ilitokea Oktoba 2023 wakati waziri wa mambo ya nje wa wakati huo wa Uturuki alipotembelea Cairo na kukutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, akithibitisha kuwa Uturuki itaimarisha uhusiano na ulimwengu wa Kiarabu.

Majadiliano zaidi yalifanyika mnamo Februari 2024 huko Ankara, ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ahmet Yildiz alikutana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waarabu Balozi Hossam Zaki, ambaye pia alishiriki katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya.

Ushirikiano rasmi ulianza na Mkataba wa Maelewano mnamo 2004 na uliimarishwa zaidi na Makubaliano ya Mfumo wa Jukwaa la Ushirikiano wa Uturuki na Kiarabu mwaka 2007.

Vilevile katika tukio muhimu nay a hali ya juu, Waziri Mkuu wa wakati huo na Rais wa sasa Recep Tayyip Erdogan alihutubia kikao cha ufunguzi cha baraza la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mnamo 2011, akiangazia dhamira thabiti ya Uturuki kwa diplomasia ya ulimwengu wa Kiarabu na kuimarisha ushirikiano wa kudumu kati ya Uturuki na Jumuiya ya Waarabu.

Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels

TRT World