Mamlaka ya Uturuki yanatumia neno "kuwakata makali " kumaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa. / Picha: AA

Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) "limewakata makali'' magaidi watatu wa PKK/KCK kaskazini mwa Iraq katika operesheni mbili tofauti, duru za usalama za Uturuki zilisema.

Idara ya ujasusi ya Uturuki ilimlenga Mazlum Ozturk, aliyepewa jina la Berxwedan Ciyager, katika operesheni ya eneo la mashambani la mkoa wa Sulaymaniyah, duru zilisema Jumatano kwa sharti la kutotajwa jina kutokana na vikwazo vya kuzungumza na vyombo vya habari.

Kama matokeo ya operesheni za MIT zinazoendelea za kukabiliana na ugaidi kaskazini mwa Syria na Iraq, vyanzo vya usalama vilisema kundi la kigaidi la PKK/KCK limelazimika kuchukua mikakati mbadala, pamoja na kuongezeka kwa juhudi kwa waajiri wapya.

Mkakati wa hivi punde wa kundi hilo la kigaidi unahusisha kuwasafirisha magaidi hadi Ulaya na kisha kuwarejesha Iraq na Syria.

Gaidi Ozturk alikuwa mmoja wao, baada ya kusafiri kutoka Uturuki hadi Ulaya Agosti 2022. Wakati wake huko Ulaya, Ozturk alihusika katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na Muungano wa Kidemokrasia wa Kurdistan wa Ulaya (KCDK-E) unaohusishwa na PKK.

Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa Ozturk alijiunga na safu za vijijini za shirika la kigaidi nchini Ufaransa mnamo Januari 2023, na baadaye kujihusisha na shughuli za kivita na kupokea mafunzo ya mbinu za mauaji zilizolenga vikosi vya usalama.

Operesheni Claw-Lock

Katika operesheni nyingine ya kukabiliana na ugaidi, magaidi wa PKK walilengwa katika eneo la Operesheni Claw-Lock kaskazini mwa Iraq na wawili waliangamizwa, Wizara ya Ulinzi ilisema Jumatano.

Mamlaka ya Uturuki inatumia neno "kuwakata makali" kumaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.

Magaidi wa PKK mara nyingi hujificha upande wa pili wa mpaka kaskazini mwa Iraq kupanga mashambulizi ya kigaidi huko Uturuki.

Ankara ilizindua Operesheni Claw-Lock mwezi Aprili 2022 ili kulenga maficho ya kundi la kigaidi la PKK katika maeneo ya Metina, Zap, na Avasin-Basyan kaskazini mwa Iraq, karibu na mpaka wa Uturuki.

Ilitanguliwa na operesheni mbili - Claw-Tiger na Claw-Eagle - iliyozinduliwa mnamo 2020 kuwaondoa magaidi waliojificha kaskazini mwa Iraqi na kupanga njama za kuvuka mpaka huko Uturuki.

Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Ututuki, Marekani na EU - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto.

TRT World