Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) limemkata makali afisa mkuu wa kitengo cha uhusiano wa kijamii la shirika la kigaidi la PKK/KCK linalohusika na eneo la Iraq/Hakurk.
Gaidi Rozerin Semzinan, kwa jina la kificho Sariye Atilla, katwa makali katika operesheni iliyofanywa kijijini Hakurk.
Semzinan, ambaye alijiunga na shirika la kigaidi mnamo 2007 na inasemekana alitoa mihadhara katika kile kinachojulikana kama vyuo vya mafunzo katika mkoa wa Haftanin kwa PKK, hivi karibuni alihusika katika shughuli za eneo la kijamii la shirika huko Hakurk, MIT ilisema.
Idara ya Ujasusi ya Uturuki ilichambua kwa uangalifu habari zote zilizotumwa kutoka kwa mawakala wa uwanjani na kwanza kutambua eneo la gaidi huyo, ambaye alifuatiliwa kwa karibu na baadaye kudhibitiwa kwa wakati unaofaa.

MIT, ambayo inaendelea kushambulia mashirika ya kigaidi katika kila kitengo, pia ilitumia oparesheni hii kupitisha ujumbe kuwa itaendelea na shughuli za wazi kama sehemu ya sera yake ya kuondoa ugaidi kutoka vyanzo katika kipindi kijacho.
Mamlaka ya Uturuki hutumia neno "kukatwa makali" kumaanisha magaidi wanaohusika walijisalimisha au waliuawa au kukamatwa.
Katika kampeni yake ya zaidi ya miaka 35 ya ugaidi dhidi ya Uturuki, PKK - iliyoorodheshwa kama shirika la kigaidi na Uturuki, Marekani, na EU - imehusika na vifo vya zaidi ya watu 40,000, ikiwa ni pamoja na wanawake na watoto.