Kampuni ya ndege ya Turkish imetambulika kwa huduma yake bora duniani /Picha : Others

Tuzo za mashirika ya ndege ya dunia zimefanywa na Skytrax .

Shirika hili lilianza uchunguzi wake wa kwanza wa kimataifa wa kuridhika kwa wateja wa usafiri wa ndege kila mwaka, kuanzia 1999

Turkish Airlines imepongezwa kwa :

  • Shirika bora la ndege barani Ulaya
  • Shirika bora la Ndege Kusini mwa Ulaya
  • Utoaji wa huduma bora kwa wasafiri katika daraja la biashara
  • Utoaji wa huduma bora kwa wasafiri katika daraja ya uchumi
  • kampuni yenye viti bora vya daraja la Uchumi barani Ulaya

Shirika la ndege la Turkish Airlines ambalo linasafiri kwa maeneo zaidi ya 300 duniani linajivunia kubeba bendera ya Uturuki kote ulimwenguni na kufungua milango kwa ulimwengu mzima kwa abiria wake.

TRT Afrika