Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan aliongea kwa njia ya simu na maafisa wa Sudan siku ya Alhamisi, akisisitiza umuhimu wa ulinzi wa maisha na mali za raia wa Uturuki na taasisi nchini Sudan huku kukiwa na mvutano katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano, Erdogan alipiga simu tofauti na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Sudan Jenerali Abdel Fettah al-Burhan, na Naibu Mwenyekiti na kiongozi wa Rapid Support Forces (RSF) Muhammad Hamdan Dagalo.

Wakati wa maongezi kwenye simu na Sudan, Rais Erdogan alisema Uturuki inafuatilia matukio ya taifa hilo ndugu la Sudan kwa wasiwasi.

Akisisitiza kuwa Uturuki wameunga mkono kwa dhati mchakato wa mpito nchini Sudan tangu mwanzo, Erdogan pia alisema matukio ya hivi karibuni yameingiliana na majadiliano ambayo yamekuwa yakiendelea tangu 2018 na kuweka mafanikio ya kipindi cha mpito hatarini.

Akizialika pande husika kusitisha mzozo na umwagaji damu na kurejea katika anga ya mazungumzo, Erdogan pia alitoa wito kwa Sudan kuchukua hatua zinazohitajika ili kuhakikisha umoja wa jamii na kutatua matatizo kwa busara na akili iliyo wazi.

Erdogan alisema Uturuki utaendelea kusimama na Sudan na watu wake katika mchakato huu, na iko tayari kutoa kila aina ya msaada, ikiwa ni pamoja na kuandaa mipango inayowezekana ya upatanishi.

Akiashiria kwamba maafisa wa Sudan wanapaswa kuzingatia ulinzi wa maisha na mali za raia na taasisi za Uturuki nchini Sudan, Erdogan pia alisisitiza kwamba hatua zinazofaa zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha matumizi salama ya Uwanja wa Ndege wa Khartoum, kuhakikisha usafirishaji wa raia wa Uturuki hadi nyumbani na kufungua njia ya dharura ya misaada ya kibinadamu.

AA