Kima cha chini cha mshahara wa watumishi wa uma kitafikia lira 22,000/ Photo: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan siku ya Alhamisi alitangaza kuongeza kima cha chini cha kila mwezi cha mshahara wa watumishi wa umma hadi lira 22,000 za Uturuki ($1.124).

"Tutapanga nyongeza ya kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma si chini ya kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma.

Mwezi Julai, kima cha chini cha mshahara wa watumishi wa umma kitafikia lira 22,000 za Uturuki," Erdogan alisema katika mji mkuu wa Ankara.

Erdogan aliongeza kuwa nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma pia "itaonekana moja kwa moja katika mshahara wa kustaafu.

"Nilimwagiza Waziri wetu kukamilisha kazi hii ifikapo Julai" alisema Rais wa Uturuki

Siku ya Jumanne, Erdogan alitangaza nyongeza ya asilimia 45% ya mishahara kwa wafanyikazi wa umma 700,00, na kuongeza kiwango cha chini cha mshahara wa kila mwezi wa wafanyikazi wa umma hadi lira 15,000 za Kituruki ($ 768).

AA