Raisi Erdogan arudi Iraq baada ya miaka 12. / Picha: A A

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili katika mji mkuu wa Iraq Baghdad kufanya mikutano na maafisa wa serikali wa Iraq.

Erdogan ameandamana na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Hakan Fidan, Waziri wa Mambo ya Ndani Ali Yerlikaya, Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Yasar Guler, Mkurugenzi wa Mawasiliano Fahrettin Altun, mshauri wake mkuu Akif Cagatay Kilic na mawaziri wengine siku ya Jumatatu.

Rais Erdogan, ambaye anazuru Iraq kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12, anatarajiwa kujadili masuala ya pande mbili na kikanda wakati wa mikutano yake na mwenzake wa Iraq Abdul Latif Rashid na Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia' al Sudani.

Pia atazuru Erbil kaskazini mwa Iraq baada ya mazungumzo ya Baghdad.

"Wakati wa ziara ya Rais Erdogan huko Erbil, haswa katika mikutano na maafisa wa serikali ya mkoa, nina imani kwamba watashiriki maono yao juu ya kuimarisha uhusiano wetu na kuhakikisha utulivu wa ndani na amani nchini Iraq," Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan alisema Jumapili katika mkutano na vyombo vya habari.

TRT World