Idadi ya watu waliokimbia makazi yao sasa imefikia takriban milioni 110, huku milioni 35.3 wakiishi kama wakimbizi nje ya nchi zao. / Picha: Jalada la AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa ujumbe kwa ulimwengu katika kuadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani, akiangazia mbinu ya Uturuki daima itakuwa "kulinda maisha na utu wa binadamu pamoja na usalama wa nchi."

"Uturuki, ambayo daima inatimiza wajibu wake wa ubinadamu na ujirani, inafanya kazi kuwezesha kurejea kwa usalama, kwa hiari, na kwa heshima kwa wakimbizi katika nchi zao, hatua muhimu ya kuchukua," alisema.

"Watu katika sehemu mbalimbali za dunia, ikiwa ni pamoja na jiografia ya nchi yetu, wanalazimika kuhama kutokana na sababu kama vile ugaidi, migogoro, vita vya wenyewe kwa wenyewe, njaa na ukame."

Rais wa Uturuki alisisitiza kuwa taifa lake limesimama kidete kuwatetea wale wanaokimbia mateso bila ubaguzi wowote kwa karne nyingi.

"Mtazamo wetu katika suala la uhamiaji usio wa kawaida na wakimbizi ambao ni changamoto ya kimataifa, ni kulinda maisha na utu wa binadamu pamoja na usalama wa nchi yetu. Taifa letu, ambalo limekuwa likiwatunza wale wanaokimbia mateso bila kuweka tofauti yoyote, kwa mara nyingine tena imeonyesha msimamo uleule wa kudhamiria kukabiliana na machafuko katika eneo letu, kutoka Syria hadi Ukraine," Erdogan alisema.

Rais alisisitiza mtazamo wa nchi yake kwa uhamiaji usio wa kawaida na wakimbizi kama changamoto ya kimataifa.

"Tunakataa matamshi ya chuki dhidi ya wakimbizi, kuenea kwa itikadi ya ki-Nazi, na chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya wageni, ambayo inakita mizizi katika nchi za Magharibi na kisha kuenea kwa jamii nyingine kama mzabibu wenye sumu.

Tunazingatia mienendo hii ya kimakusudi ambayo haizingatii mtu yeyote ambaye ni tofauti katika suala la rangi, utamaduni, au imani kama tishio kwa maadili ya kibinadamu na mustakabali wa pamoja wa ubinadamu."

"Tunatoa wito kwa pande zote kufanya juhudi zaidi"

Akiangazia athari za mawazo ya kikoloni, Rais Erdogan aliashiria mabadiliko ya Bahari ya Mediterania kuwa kaburi kubwa la wakimbizi katika miaka ya hivi karibuni.

"Mawazo ya kiburi yenye mizizi ya kurudi kwenye ukoloni imekuwa na athari kubwa kwa Mediterania, ambayo imekuwa chimbuko la ustaarabu katika historia, na kugeuka kuwa kaburi kubwa la wakimbizi katika miaka ya hivi karibuni."

"Mkasa wa kibinadamu uliotokea wiki iliyopita katika Bahari ya Aegean, ambapo mamia ya watu wasio na hatia, wengi wao wakiwa watoto, walipoteza maisha yao hadharani, ni mfano wa hivi karibuni na wa aibu zaidi."

Alisisitiza umuhimu wa mkataba wa kimataifa wa wakimbizi, uliopitishwa Disemba 2018 na michango hai ya Uturuki, katika kutatua suala la wakimbizi. Alitoa wito kwa pande zote husika kuongeza juhudi katika kutekeleza mkataba na kutimiza wajibu wao.

"Jumuiya ya kimataifa, hasa nchi zinazokemea wengine kuhusu haki za binadamu na demokrasia, lazima sasa ziwajibike. Suala la wakimbizi linaweza kutatuliwa kwa kuondoa sababu kuu za uhamiaji na kulazimishwa kuhama. Mafanikio na utekelezaji wa mkataba wa kimataifa wa wakimbizi ni muhimu sana katika suala hili," Rais alisema.

"Tunatoa wito kwa pande zote husika kufanya juhudi zaidi katika utekelezaji wa Mkataba na kufuata majukumu."

Rais Erdogan alihitimisha ujumbe wake kwa kueleza matumaini kuwa Siku ya Wakimbizi Duniani itachangia katika kutatua changamoto zinazowakabili wakimbizi duniani kote.

"Kwa uchunguzi na matakwa haya, ninatumai kuwa Siku ya Wakimbizi Duniani itachangia katika kujenga uelewa wa kimataifa, kuzuia majanga mapya, na kutatua matatizo ya wakimbizi wote wanaohangaika kwa ajili ya kuishi katika pembe tofauti za dunia."

TRT World